Saturday 4 October 2014

MAGONJWA YENYE UHUSIANO NA UKIMWI KATIKA MAENEO YA KINYWA NA USO.

Ukimwi  “upungufu wa kinga mwili”, ni ugonjwa unaoshambulia na kuua chembe chembe nyeupe za damu zinazosaidia mwili kupambana na magonjwa. Kutokana na upungufu huu wa kinga, magonjwa nyemelezi huanza kumpata muathirika wa ukimwi. Magonjwa yatokanayo na ukimwi uweza kujidhihirisha sehemu mbali mbali za mwili ikiwemo eneo la kinywa na uso. Kwa sasa nitaandika juu ya magonjwa ya eneo la kinywa na uso.

                                                  1. Fangasi za mdomoni (oral candidiasis)
Ugonjwa huu hujidhihirisha kama utando mweupe kwenye ulimi, paa la kinywa au kuta za kinywa, utando huu ni rahisi kukwanguliwa na kuacha ngozi laini yenye vipele vipele vyekundu. Wakati mwingine uonekana kama vipele vipele vyeupe kwenye kinywa.
Matibabu: Ugonjwa huu hutibika kwa kutumia dawa za kawaida za fangasi, ziwe vidonge, za maji au za kumun’gunya katika hali ya gel
                                                               2. kapos's sarcoma

chembe chembe zinazotengeneza ngozi ya ndani ya mishipa ya damu.
Kansa hii ilikuwepo tangu zamani lakini imeongezeka kwa kasi baada ya kugundulika kwa Ukimwi. Tafiti nyingi kwa sasa zinaonyesha kansa hii ina uhusiano mkubwa na Ukimwi.
Kansa hii kwenye kinywa inajidhihirisha kama uvimbe tepetepe wenye rangi ya zambarau japo wakati mwingine nyekundu damu ya mzee.
Wakati mwingine yawezekana usiwe uvimbe bali eneo fulani la ngizi zilizo tanda kinywa kubadilika rangi na kuwa zambarau au nyekundu.
Kansa hii inaweza jitokeza sehemu yoyote mdomoni, kama kwenye ulimi, kuta za kinywa, paa la kinywa na kwenye fizi na hata kwenye tonsili.
Nje ya kinywa kwenye uso, kansa hii hushambulia mitoki iliyo chini ya kidevu na kwenye shingo. Mitoki uvimba bila sababu ilyo wazi (kwa kawaida mitoki uvimba kama kuna kidonda sehemu fualani au ugonjwa).
Matibabu: Kwa wagonjwa wa Ukimwi kansa hii ikijitokeza ni miongoni wa sababu za kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi hata kama kinga yako bado iko juu. Matibabu yanaweza kuwa upasuaji kuondoa uvimbe, mionzi kuunguza chembe chembe za kansa, dawa za kansa au muunganiko wa njia njia mbili kati ya hizo au zote kwa pamoja.
3. Magonjwa ya fizi
Kwa kawaida magonjwa ya fizi huwapata watu wasiopiga mswaki au wanaopiga mswaki isivyo paswa. Mara nyingi utakuta mtu mwenye magonjwa haya meno yakiwa na tando za uchafu na wadudu (dental plaque) au hata ugaga uliojishikiza kwenye meno kama miamba (calculus). Lakini kwa mgonjwa wa ukimwi waweza kuta kinywa ni kisafi lakini fizi zimejaa vidonda vidonda, na vidonda hivi husambaa kwa kasi.
Magonjwa haya fizi hushambulia pia mifupa inayoshikilia mizizi ya meno hivyo kupelekea meno kulegea na hatimaye kutoka
Matibabu: Kusafisha meno na kutumia dawa za antibiotic za kusukutua na vidonge vya kumeza.
                                         4. Kuvimba kwa tezi kubwa la mate lililopo jirani na sikio (parotid     salivary gland enlargement)
Huku ni kuvimba hadi kuonekana kwa tezi la mate lililopo jirani ya sikio. Kwa kawaida tezi ili halionekani, hivyo ukiliona limevimba jua kuna tatizo. Ugonjwa huu huenda sambamba na kukauka kwa kinywa, kwani matezi haya ndiyo hutoa kiwango kikubwa cha mate mdomoni. Unaweza kuvimba tezi la upande mmoja au pande zote mbili.
Matibabu: Ugonjwa huu huweza kujiponea wenyewe lakini wakati mwingine yaweza kuhitaji matibabu.
 

No comments:

Post a Comment

.