Friday 24 October 2014

JINSI YA KUTAMBUA NA KUDHIBITI UGONJWA WA PRESHA MAPEMA.

Presha ya Juu hutokea endapo itazidi kiasi cha140/90mmlHg na ikiwa haitibiwi huharibu mishipa ya damu katika macho, misuli ya moyo kuwa minene , kusababisha mshutuko wa  moyo (heart attack), mshipa ya damu safi kuwa migumu, figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure) na kiharusi (stroke).  Presha kwa mwanamke mjamzito inaweza kusababisha kifafa cha mimba na kufanya hata kiumbe kufa tumboni. Hivyo ni muhimu kuchunguza presha ya wanawake wote wajawazito.

Visababishi vya presha kuwa juu

Chuvi nyingi
Unene uliozidi
Umri mkubwa au uzee
Magonjwa ya Figo
Historia ya ugonjwa wapresha kwenye familia
Ugonjwa wa kisukari
Ujauzito

Dalili ya mtu mwenye ugonjwa wa presha
Mara nyingi presha haina dalili hadi ilete madhara na hivyo huitwa( silent killer ) muuaji wa kimyakimya
kichwa kuuma
kizunguzungu
kubanwa na pumzi
kutokuona vizuri
kichevuchevu


Vitu vinavyo changia hali presha kuwa mbaya zaidi ni
Kula chuvi nyingi
Unene uliozidi
Kutofanya mazoezi mara kwa mara
Kunywa pombe nyingi
Uvutaji wa sigara

Tiba ya ugonjwa wa presha

Moja wapo ya tiba ya presha ni kuacha vyakula vyenye chumvi kabisa kama itatumika iweke kidogo ya ladha wakati chukula kipo jikoni.
Pia mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ni muhimu kwa tiba ya ugonjwa wa presha. Jitahidi kutenga mda wa mazoezi angalau dakika 30-60 mara tatu kwa wiki.
Epuka vyakula vyenye mafuta na lehemu maana vinaganda kwenye mishipa ya damu na kusababisha presha.
Kula matunda na mboga za majani mara kwa mara
Daktari atakapo baini kuwa presha yako ipo juu, kulingana na aina na kiwango cha presha atakushauri kuhusiana na vyakula na jinsi ya kubadili mwenendo wa maisha au atakuanzishia dawa mara moja. Ni muhimu uelewe kuwa utakao anzishiwa dawa hutakiwi kuziacha maisha yako ote vinginevyo hali ya presha itarudi kama mwanzo.


No comments:

Post a Comment

.