Sunday 26 October 2014

JE…UNAFAHAMU KUHUSU TETEKUWANGA (CHICKENPOX) ??

Ni ugonjwa wa ngozi unaotokea hasa wakati wa utoto na unasababishwa na kirusi aina ya varicella-zoster

Watu hupata ugonjwa huu Zaidi katika umri wa miaka 15,na wengi Zaidi kati ya miaka 5 hadi 9,ingawa katika umri wowote unaweza ukapata matetekuwanga

Ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi Zaidi.



NJIA ZINAZOAMBUKIZA
1.Njia ya hewa
2.kugusana na majimaji yanayotokea wakati wa kupasuka kwa malengelenge
3.kugusana na vifaa au nguo ambazo zimegusana na majimaji ya malengelenge
4.matonetone wakati wa kupumua (droplets in exhaled air)

DALILI
1.Siku moja hadi mbili za homa kiasi
2.Mwli kuchoka na kuishiwa nguvu
3.kukosa hamu ya kula (Anorexia)
4.vipele vyenye kujaa maji kama malengelenge

Mara nyingi vipele hivi huanzia kichwani kuelekea katika sehemu ya mwili (trunk) na kisha katika mikono na miguu

Vipele hivi vinaambatana na muwasho mkali


MARA UONAPO DALILI HIZI FIKA KATIKA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA YA AFYA KWA MATIBABU ZAIDI

No comments:

Post a Comment

.