Unene kupita kiasi husababishwa kuwa na mafuta mengi
mwilini kutokana na kukosa
mazoezi ya kutosha au kula chakula kupita kiasi ambacho ukosa matumizi na
kuifadhiwa kwenye tumbo, makalio, maziwa au kiungo chochote laini. Hii pia
inaweza kuchangiwa na mabadiliko ya hormone asa kipindi cha ujana, uzeeni au
ujauzito na kurithi katika familia.
Tatizo ili hukuweka katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo
na ini, kiharusi, shinikizo la damu, kisukari, kukoroma usiku, maumivu katika joint
za mifupa, kushindwa kupumua vizuri na saratani.
MATIBABU YAKE
1. Kupanga lishe na mazoezi ni tiba tosha ya tatizo ili. Epuka
vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na kula vyenye nyuzinyuzi , matunda na
nafaka.
2. Juice ya limao glasi moja kila asubuhi ni njia raisi ya
kupambana na unene huu kwani hurekebisha mfumo wa chakula, damu na kuondoa sumu
mwilini.
3. Juisi ya mshubiri ikichanganywa na machungwa kila asubuhi
kwa muda wa mwezi mmoja husaidi kuondoa mafuta ya ziada mwilini.
4. Kijiko kimoja cha asali katika kikombe cha chai kila siku
husaidia kupunguza mafuta mwilini.
5. Unaweza pia kupunguza kulala mchana, kukaa kwenye sofa au
kukalia viti laini kwa muda mrefu
Kunywa maji ya moto badala ya baridi husaidia kuondoa mafua
ya ziada kwenye mishipa ya damu.
LIKE PAGE YETU FACEBOOK USIPITWE NA MENGI ZAIDI KUHUSU AFYA YAKO.
LIKE PAGE YETU FACEBOOK USIPITWE NA MENGI ZAIDI KUHUSU AFYA YAKO.
No comments:
Post a Comment