Tuesday, 2 September 2014
UMUHIMU WA KUOTA JUA ASUBUHI
Watu wengi huwa na upungufu wa vitamini D kwasababu hawatoki nje kupata mwanga wa jua ambao huchochea seli katika ngozi ya mwili wako kuzalisha Vitami D inayoboresha afya ya mifupa na meno na kukukinga na hatari ya kushambuliwa na magonjwa ya moyo, kisukari na saratani.
Vitamini hii utunzwa chini ya ngozi na usaidia mwili kufyonza madini ya kalsiumu kutoka tumboni ambayo uimarisha na kuzuia kulika au kuvunjika kwa mifupa na kutengenezwa kwa insulini ambayo usaidia kupunguza sukari mwilini. Ikumbukwe pia kwa wale wazembe wa kuota jua la asubuhi vitamini hii pia inaweza kupatikana kwenye mayai, samaki, maziwa, maini, nafaka na uyoga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment