Saturday 16 August 2014

ATHARI ZA KUTUMIA CHUMVI NYINGI KATIKA CHAKULA.

Mara nyingi tumekuwa tukishauriwa kupunguza kiasi cha chumvi kwenye chakula si tu kwa wagonjwa wa kisukari, figo, moyo, ini na presha bali hata kwa mtu mwenye afya nzuri anatakiwa kupunguza kiasi cha chumvi kwa huweza kusababisha matatizo yafuatayo:-

  • Magonjwa ya figo, utumiaji wa chumvi kupita kiasi uongeza kiasi cha sodiamu mwilini ambayo huzuia figo kutoa maji ya ziada mwilini na kuongeza presha ya damu ambayo huaribu figo na utendaji wake wa kazi na kushundwa kuchuja damu na kutoa sumu mwilini.
  • Kuharibu mishipa ya damu,chumvi uongeza sodiamu ambayo uongeza mzigo ndani ya mishipa ya ateri zenye misuli midogo na hivyo huweza kupasuka na kusababisha sehemu nyingine za mwili kukosa damu yenye virutubisho na oksijeni.
  • Magonjwa ya moyo, chumvi huongeza presha ambayo uharibu mishipa ya moyo na kuongeza mapigo ya moyo na hivyo kusababisha maumivu makali kwenye kifua(Anjaina) na ikiendelea kwaa muda mrefu mishipa huziba au kupasuka sambamba na moyo kuwa mkubwa.
  • Matatizo kwenye ubongo, chumvi huongeza presha ambayo uharibu mishipa ya damu kwenye ubongo na kusababisha matatizo ya akili na kiharusi.
  • Pia huweza kusababisha matatizo mengine au kuongeza madhara ya kisukari, mawe kwenye figo, kansa ya tumbo, unene kupita kiasi, maumivu ya kichwa na magonjwa ya mifupa.


No comments:

Post a Comment

.