Homa ya mapafu au Pneumonia ni ugonjwa unaosababishwa na wadudu, virusi, fangasi na bakteria kama Escherichia, streptococci, RSV, Streptococcus pneumoniae, Mycoplasma pneumoniae,kifaduro, na virusi vya mafua ambao ushambulia njia ya hewa na mapafu asa kwa watoto wadogo chini ya miaka miwili.
Dalili za ugonjwa wa homa ya mapafu
Dalili za kawaida za homa ya mapafu ambazo huwapata karibu watoto wote
wanaoathirika na ugonjwa huu ni pamoja na:- homa
- Kuhisi baridi
- kikohozi
- Kupumua kwa haraka kuliko kawaida
- kutoa sauti isiyo ya kawaida wakati wa kupumua
- Mbavu za mtoto kuingia ndani wakati wa kupumua
- maumivu ya tumbo
- kupoteza hamu ya kucheza
- kupoteza hamu ya kula na kushindwa kunyonya
- Mtoto kubadilika rangi na kuwa na rangi bluu katika midomo na kucha
- Hata hivyo, si lazima dalili zote hizi ziwepo kwa kila mtoto. Baadhi ya watoto huonesha kupumua kwa haraka kama dalili pekee ya homa ya mapafu.
- Iwapo vimelea vimeshambulia sehemu za chini ya mapafu karibu ya tumbo, sehemu ijulikanayo kama kiwambo au diaphragm, mtoto anaweza asioneshe hali yeyote ya kushindwa kupumua ingawa anaweza kuwa na homa na kujihisi maumivu makali ya tumbo, vichomi na pia kutapika.
- Watoto wachanga wanaweza kushindwa kunyonya, na pia kupoteza fahamu na kupata degedege.
Matibabu
Maamuzi ya Matibabu kwa watoto
wenye homa ya mapafu hutegemea aina ya vimelea, umri na hali ya mtoto. Mara
nyingi dawa za maji na sindano za erythromycin, benzylpenicillin, cefotaxime, amoxycillin, clarithromycin nk hutumika kutibu homa na maambukizi huku dawa za paracetamol na diclofenac hutumika kushusha homa ya mwili.Kumbuka antibiotics hazina uwezo wowote wa kutibu homa inayosababishwa na virusi hivyo hupona kwa kutumia tu dawa za kushusha homa, lishe, mazingira yenye hewa safi. na kumpa mtoto maji mengi. Ieleweke kuwa ni tabibu anayeweza kufahamu kama mtoto wako anahitaji antibiotics au dawa za aina nyingine, kwahiyo ni muhimu kwa mzazi ama mlezi kumpeleka mtoto hospitalini haraka pindi mtoto anapoonesha dalili za ugonjwa huu badala ya kuamua kumpa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.
No comments:
Post a Comment