NINI HUSABABISHA?
Baadhi ya sababu zinazopelekea hali hii ni pamoja na:
- Kufunga au kukosa choo kwa muda mrefu
- Kupata choo kigumu
- Ujauzito katika kipindi cha miezi 6
- Uzito kupindukia
- kuwa na kuta na mishipa dhaifu ya njia ya haja kubwa
- Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
- kutokula vyakula vyenye nyuzinyuzi
DALILI
Dalili za tatizo hili ni pamoja na:
- Maumivu katika sehemu ya haja kubwa
- Kuwasha na kujikuna katika njia ya haja kubwa
- Kutoa kinyesi chenye damu au Kutokwa damu kila baada ya haja kubwa
- kuhisi kurudi haja kubwa hata mara baada ya kujisaidia
- Uvimbe katika sehemu ya haja kubwa
MATIBABU (WASILIANA NASI KUPATA DAWA HIZI)
Matibabu ya tatizo hili ni sambamba na kuhakikisha unapata choo laini na kuondoa uvimbe katika njia hii ambayo ni pamoja na:
- Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi sambamba na matunda na mboga za majani na nafaka
- Jitahidi kwenda haja mara kwa mara kila unapohisi kufanya hivyo na sio kuibana
- Kula mlo kamili sambamba na maji mengi kila siku
- Tumia toilet paper yenye unyenvu ili kulainisha sehemu hii na iweke safi muda wote
- Unaweza kutumia dawa ambazo usaidia kulainisha njia hii na kuongeza hamu ya kwenda chooni
- kama itashindikana unaweza kwenda hospitali kwa uchunguzi na ushauri zaidi ambapo upasuaji aina ya haemorrhoidectomy huweza kufanywa ili kuondoa tatizo hili.
No comments:
Post a Comment