Zaidi ya asilimia 78 ya wanawake hupata maambukizi ya fungus sehemu za siri mara moja au zaidi katika maisha. Hata hivyo baadhi hupata maambukizi mara kwa mara.Maambukizi hufanya na aina ya fangas waitwa Candida albicans. Fangasi hawa kwa kawaida hupatika katika njia ya uzazi ya mwanamke bila madhara yoyote, lakini mabadiliko ya hormoni na upungufu wa kingi mwilini sambamba na maambukizi mbalimbali huweza kusababisha ugonjwa.
DALILI
Ugonjwa huu unaweza kuwa na dalili mbalimbali
Mgonjwa anaweza kusikia miwasho, kuchubuka sehemu za siri, kusikia
maumivu wakati wa kujamiiana au wakati wa kukojoa na pia kutoa uchafu
mweupe kama maziwa mgando ambao kwa kawaida hauna harufu.
Pi dalili hizo zinaweza kuambatana na kuvimba mashavu ya njia ya uzazi, kidonda au mipasuko.
MATIBABU
Dawa za aina tofauti kama clotrimazole miconazole fluconazole nystatin na fluconazole zinaweza kutumika kutibu ugonjwa huu kwa muda wa siku 5 mpaka 14 kutokana na ukubwa wa tatizo.. Dawa
zinaweza kuwa za kutumbukiza kwenye njia ya uzazi wa
mwanamke, kupaka(cream) na wakati mwingine mgonjwa
anaweza kuandikiwa dawa za kumeza iwapo amekuwa akipata ugonjwa huu mara
kwa mara.
Pia epuka kuvaa ngua za kubana na kuacha unyevunyevu sehemu za siri sambamba na kufanya usafi mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment