Wednesday, 9 July 2014

Ugonjwa wa Mtoto Jichoni (Cataracts)

Mtoto jichoni ni nini?
Huku ni kuwa na mawingu kewnye kioo asili cha jicho (natural lens) kioo hiki ndicho hukuwezesha kuelekeza mishale ya nuru ili kutoa sura ilizo dhahiri. Huweza kutokea katika jicho moja au yote na husambaa kutoka jicho moja hadi lingine.
Baadhi ya mambo yanayosababisha mtoto jichoni ni:
  • Kukaa mahali palipo na mwanga mwingi kwa miaka mingi au kazi inayokufanya kukaa hapo.
  • Kisukari
  • Dawa za ugonjwa wa pumu
  • Kufuta sigara au kunywa pombe
  • Kuzaliwa na mtoto wa jicho hasa katika macho yote
  • Uzee
  • Matatizo mengine ya macho kama vile Glaucoma.
Dalili ni zipi?
  • Kuona mawingu-wingu/weupe mbooni ya jicho (pupili)
  • Marangi huonekana kama yamefifia.
  • Mwangaza huukuumiza macho au unaonekanana mkali sana.
  • Unaona miviringo kwenye mwangaza wakati wa usiku.
  • Huoni vizuri sana usiku
  • Aina ua miwani hugeuzwa mara kwa mara.
Utazuia Mtoto Jichoni aje?
  • Valia miwani yakupunguza mwangaza au kofia.
  • Acha kufuta sigara
  • Kula chakula kitakachokupa afya.
  • Kaguliwa macho na mboo ya jicho lako ipanuliwa kama umezidi miaka 60.
Utatibiwa aje?
Ita daktari wako atakayekueleza kwa mtaalamu wa macho aangalia dalili ulizo nazo. Unaweza kutibiwa kama kwa:
  • Kupatiwa miwani mpya.
  • Kuongezewa mwangaza
  • Miwani ya kupunguza mng’ao
  • Kufanyiwa upasuaji kama uwezo wa kuona unaubadili mtindo/desturi yako.


KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI

No comments:

Post a Comment

.