Tatizo hili la uvimbe ambao sio saratani huwatesa wakina
mama na wasichana wengi na hivyo kufikia hatua ya kuondolewa kizazi endapo
hautowaiwa na kutibiwa katika dalili za awali. Ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa fibroids au
leimyoma na huathiri zaidi ya asilimia 25 ya wanawake wa kiafrica na asilimia 50
ya wazungu. Uvimbe huu huwa katika umbile la misuli laini na myembamba na hukua
siku hadi siku kutokana na vichocheo vya estrogeni hasa kipindi cha hedhi na
ujauzito.
Uvimbe huu hujitokeza
katika ukuta wa kati, wa nje, au ndani kabisa ya nyumba ya uzazi na huambatana
na dalili zifuatazo.
UVIMBE NJE YA NYUMBA YA UZAZI
Husababisha maumivu ya maumivu chini ya kitovu, mgongo na
miguu.
UVIMBE KATIKATI YA
NYUMBA YA UZAZI
Husababisha kutoka na damu nyingi na nzito kipindi cha hedhi
,maumivu chini ya kitovu na mgongoni, na tumbo kujaa gesi na kukojoa mara kwa
mara au kukosa choo.
UVIMBE NDANI YA NYUMBA YA UZAZI
Hii hutokea mara
chache na husababisha matatizo makubwa sana kama kutokwa na damu nzito au hedhi
isiyokata na yenye maumivu kwa muda mrefu.
Dalili nyingine ni pamoja na matatizo wakati wa kujifungua,
kuharibika kwa mimba mara kwa mara, tumbo kuvimba chini ya kitovu, maumivu
makali wakati wa tendona upungufu wa damu.
MATIBABU
Matibabu ya tatizo ili ni pamoja na dawa za kupunguza uvimbe
na upasuaji kuondoa kizazi au uvimbe kutokana na mahitaji ya mgonjwa.
Mchanganyiko wa dawa kama GNRTHAs, HRT, tranexamic acid, mefanamic acid,
levonorgestrel na ibuprofen huweza kutumika kupunguza uvimbe na maumivu kutokana
na ukubwa wa tatizo kwa maelekezo ya daktari.
Tiba ya upasuaji ufanyika pale dawa zinaposhindwa kumaliza
tatizo ambao uhusisha kuondoa kizazi(hystrectomy) na kuondoa uvimbe(
myomectomy) kutegemea na umri wa mgonjwa. Idadi ya watoto na maamuzi yake binafsi.
Hata hivyo wataalamu wa afya wanashauri wanawake wote
kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara ili kubaini maradhi hatari yanayoweza
kuzuilika au kutibika mapema.
KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA
HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI
No comments:
Post a Comment