Visababishi vya presha kuwa juu
- Chuvi nyingi
- Unene uliozidi
- Umri mkubwa au uzee
- Magonjwa ya Figo
- Historia ya ugonjwa wapresha kwenye familia
- Ugonjwa wa kisukari
- Ujauzito
Dalili ya mtu mwenye ugonjwa wa presha
Mara nyingi presha haina dalili hadi ilete madhara na hivyo huitwa( silent killer ) muuaji wa kimyakimya
- kichwa kuuma
- kizunguzungu
- kubanwa na pumzi
- kutokuona vizuri
- kichevuchevu
- Kula chuvi nyingi
- Unene uliozidi
- Kutofanya mazoezi mara kwa mara
- Kunywa pombe nyingi
- Uvutaji wa sigara
Tiba ya ugonjwa wa presha
- Moja wapo ya tiba ya presha ni kuacha vyakula vyenye chumvi kabisa kama itatumika iweke kidogo ya ladha wakati chukula kipo jikoni.
- Pia mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ni muhimu kwa tiba ya ugonjwa wa presha. Jitahidi kutenga mda wa mazoezi angalau dakika 30-60 mara tatu kwa wiki.
- Epuka vyakula vyenye mafuta na lehemu maana vinaganda kwenye mishipa ya damu na kusababisha presha.
- Kula matunda na mboga za majani mara kwa mara
- Daktari atakapo baini kuwa presha yako ipo juu, kulingana na aina na kiwango cha presha atakushauri kuhusiana na vyakula na jinsi ya kubadili mwenendo wa maisha au atakuanzishia dawa mara moja. Ni muhimu uelewe kuwa utakao anzishiwa dawa hutakiwi kuziacha maisha yako ote vinginevyo hali ya presha itarudi kama mwanzo.
No comments:
Post a Comment