Maafisa wa afya wanatahadharisha juu ya utumiaji wa muda mrefu wa dozi
kubwa ya dawa za kuondoa kiungulia, (heartburn) na kusisitiza kwamba
zinasababisha mifupa kupasuka. Dawa hizo ni zile zinazojulakana kama
Proton Pumping Inhibitors (PPI) zinazozuia kiungulia na ambazo hutumiwa
kudhibiti kiwango cha asidi katika tumbo na pia kutibu ugonjwa wa GERD
au gastroesophageal reflux disease. Taarifa hizo zilizotolewa na Kitengo
cha Kusimamia Vyakula na Dawa cha Marekani (FDA) zinasema kwamba, dawa
hizo za kingulia huongeza uwezekano wa kupasuka mifupa ya nyonga (hip),
mikono na ute wa mgongo kwa watu wazima, hasa iwapo dawa hizo
zitatumiwa kwa mwaka mmoja au zaidi, au kwa dozi kubwa.
Joyce Korvick
Mkurugenzi wa masuala ya usalama wa kitengo cha FDA anasema kwamba, kwa
kuwa dawa hizo zinatumiwa sana na watu wengi, ni muhimu kwa watu wote
kufahamu madhara yanayoweza kusababishwa na dawa hizo. Maafisa hao pia
wamewataka madaktari kuwaandikia tu dawa hizo wagonjwa ambao hali zao ni
mbaya mno, na kusisitiza kuwa faida ya dawa hizo pale zinapotumiwa mara
chache ni zaidi ya hatari inayozisababisha.
Huko nyuma pia wataalamu
walisema kwamba, dawa hizo za kutibu kiungulia zinahusiana na ongezeko
la hatari ya maambukizo ya bacteria aina ya C. difficile anayesababisha
ugonjwa wa kuharisha.
Dawa hizo ni kama zile za Emsomeprazole,
Dexlansoprazole, Lansoprazole, Emprazole/Sodium Bicarbonate,
Pantoprazole, Rabeprazole na Rabeprazole.
Ndugu mdau kama wewe ni miongoni mwa wanaotumia dawa hizo, basi jihadhari kabla ya hatari!
No comments:
Post a Comment