Tatizo la kukosa choo au kuwa na choo kigumu kwa watoto wadogo (Constipation)
Watoto
wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa
vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu
au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation. Hali hiyo
huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa
maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine
zaidi ya maziwa. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa
hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale
wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama
ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda
mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.
Mtoto mwenye tatizo la
kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na
kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku
akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini
ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.
Iwapo mtoto wako mchanga
au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza
wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari.
Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:
1. Jaribu kumpa mtoto wako
maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au
ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni
bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.
2. Iwapo maji
hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya
tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na
safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au
ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa.
3.
Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele (fibers). Iwapo mwanao
ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko
vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple
na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto
cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au
kufunga choo.
4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.
5.
Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili
kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil)
au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la
kukosa choo la mtoto.
6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa
kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva
katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako
hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya
kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine
kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.
7. Kuna
baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na
kutumia maziwa ya ng’ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya
kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya
ng’ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha
choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo
halisababishwi na maziwa ya ng’ombe.
8. Mwogeshe au mweke mwanao
katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi
kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo
husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa
urahisi.
N.B Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati
huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract,
saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto
huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.
Utafiti
unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na
kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa
mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia
upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.
No comments:
Post a Comment