Tunda la stafeli kuwa na uwezo
mkubwa wa kutibu magonjwa hatari, ukiwemo ugonjwa wa saratani. Hata
hivyo, utafiti wa kwanza kuonesha uwezo wa stafeli kutibu saratani,
uligundulika tangu miaka ya sabini, lakini ulifanywa siri hadi hivi
karibuni ulipowekwa bayana tena.
Hivi
sasa wakereketwa wa tiba mbadala na dunia kwa ujumla, wanafahamu kuwa
stafeli lina virutubisho vyenye uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa ya
saratani kushinda hata dawa za kisasa. Tunda hili linapatikana nchini
kwa wingi, mjini na vijijini. Kwa lugha za kigeni linajulikana pia kama
Soursop au Graviola.
VIRUTUBISHO VILIVYOMO
Kwa mujibu wa tafiti za
kisayansi, stafeli limesheheni idadi kubwa ya virutubisho ambavyo ni:
Amino Acid, Acetogenins, Vitamin C, Iron, Riboflavin, Phosphorus,
Thiamine, Calcium, Carbohydrates, Niacin na Fibers na vingine vingi.
SARATANI NA STAFELI
Ingawa suala la stafeli peke
yake kutibu saratani lina mjadala, lakini hakuna shaka kabisa kuwa lina
virutubisho vyenye uwezo wa kupambana au kupunguza makali ya saratani.
Ukweli uliogundulika hivi karibuni, umewapa wagonjwa wa saratani njia
nyingine mbadala ambayo haikuwepo hapo awali. Kwani hivi sasa wanaweza
kulitumia stafeli kama dawa ya kupunguza makali au kuwapa kinga dhidi ya
saratani na wanaweza pia kuitumia pamoja na matibabu wanayopewa ya
mionzi na kupata ahueni kubwa.
USHAHIDI WA KIMAABARA
Zaidi ya majaribio 20 ya kimaabara yaliyofanywa kuhusu uwezo wa stafeli, yamebaini haya yafuatayo:
Stafeli huua chembechembe za saratani (cancerous cells) aina 12, ikiwemo saratani ya matiti, mapafu, kongosho, kibofu na tumbo.
Stafeli
lina mchanganyiko wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa seli za
saratani mara 10,000 zaidi ya dawa ya ‘Adriamycin’ ambayo ndiyo hutumika
kutibu aina mbalimbali ya saratani.
Mchanganyiko wa virutubisho vya
‘Annonaceous’ ‘Acetogenins’ vilivyomo kwenye stafeli huua seli (cells)
zilizoathirika tu na saratani, tofauti na dawa za kisasa ambazo zenyewe
huua seli zilizoathirika na hata zisizoathirika.
Stafeli hudhibiti
ukuaji wa seli za saratani bila kusababisha madhara mengine kama ilivyo
kwa dawa za kisasa, ambazo wakati mgonjwa anapozitumia, iwe zile za njia
ya mionzi, sindano au vidonge, huwa zina athari mbaya kwa mtumiaji na
wakati mwingine huweza kumsababishia matatizo mengine ya kiafya.
UMUHIMU WA STAFELI KWA WANAOTUMIA TIBA YA KISASA
Mgonjwa
wa saratani anayetumia tiba ya hospitali anashauriwa pia kula sana
stafeli kwani lenyewe husaidia kupunguza makali ya dawa anazotumia.
Imetoka: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/stafeli-lina-uwezo-wa-ajabu-wa-kutibu-magonjwa-hatari
No comments:
Post a Comment