Saratani ya maziwa ni moja ya magonjwa yanayoongoza katika kusababisha vifo kwa kina mama duniani. Lakini licha ya ugonjwa huo kuwa tishio iwapo tutajizoeza kujipima sisi wenyewe mara kwa mara ili kuangalia iwapo tuna dalili za ugonjwa huo, suala hilo linaweza kusaidia kutambua uwepo wa ugonjwa huo mapema na kuanza matibabu haraka, na hivyo kuepusha vifo vya mamilioni ya wanawake duniani kila mwaka. Kutokana na idadi kubwa ya vifo na kesi za kansa ya matiti duniani, wataalamu wanatuambia kuwa, utambuzi wa awali husaidia kupunguza vifo na mateso yanayotokana na ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa. Pia utambuzi wa mapema wa ugonjwa huo hupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa na hata serikali huika. Kwa mfano nchini Tanzania , rekodi za hospitalini zinaonesha kuwa, kila mwaka wanawake 2,500 wa nchi hiyo wanaripotiwa katika hospitali kuu wakisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya matiti. Kati ya hao 2,500, wanawake 300 tuu ndo wanaoweza kuendelea na matibabu ya mionzi au upasuaji wa ugonjwa huu kupitia wataalamu wa ugonjwa huo nchini humo. Lakini wanaobakia ambao ni wengi huwa hawawezi kuendelea na tiba kutokana na kushindwa kugharamia tiba ya ugonjwa huo na sababu nyinginezo. Mara nyingi na kwa bahati mbaya wagonjwa wengi mara wanapogundua kwamba wana kansa ya matiti huwa tayari ugonjwa huo hatari umeshasambaa katika mwili na mishipa ya limfu na hivyo wataalamu wa tiba huwa na muda mchache wa kumsaidia mgonjwa, na mara nyingine pia baada ya kipindi kifupi mgonjwa huwa katika steji za mwisho za ugonjwa huo. Yote hayo yanaonesha umuhimu wa kila mwanamke kufahamu namna ya kujichunguza ili kufahamu kama ana ugonjwa huo au la.
Tafiti zinaonyesha kwamba, ingawa watu wa umri wote wako katika hatari ya kupatwa na kansa ya matiti lakini ugonjwa huo unawapata zaidi wanawake baada ya umri wa miaka 40 na kuendelea. Lakini hii haimaanishi kwamba wanawake walio chini ya umri huo hawapaswi kujichunguza mara kwa mara ugonjwa huo. Wataalamu huwashauri wasichana wawe na mazoea ya kujichunguza matiti yao toka wakiwa wadogo na kuangalia iwapo kuna mabadiliko yanayoweza kuashiria uwepo wa ugonjwa huo. Pia wanawake wote wanashauriwa kujifanyia wenyewe uchunguzi wa kansa ya matiti kwa uchache mara moja kwa mwezi. Wataalamu wanasema kuwa, asilimia 40 ya kesi za ugonjwa wa kansa ya matiti hugunduliwa na wanawake kwa huhisi uvimbe, hivyo mazoea ya kujifanyia uchunguzi ili kuangalia kama wamepatwa na ugonjwa huo ni jambo muhimu sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kipimo cha mammography kinaweza kumsaidia mwanamke kugundua kensa kabla ya kufanya uvimbe, lakini kujichunguza mwenyewe kunamsaidia mwanamke kuwajuza mapema wataalamu wa afya iwapo ataona mabadiliko yoyote yanayoweza kusababishwa na kansa ya matiti. Tunashauriwa kuwa, muda bora wa kufanya breast self examination ni siku 3 hadi 5 baada ya kuanza hedhi. Namna ya kujichunguza matiti au breast self exam ni kama ifuatavyo. Kwanza kabisa ni vizuri zaidi uchunguzi huo ukifanywa wakati mtu akiwa amelala kwenye kitanda au akiwa mbele ya kioo kinachoweza kuonesha vizuri kiwiliwili hasa upande wa juu. Kama umesimama nyoosha mkono wako na kuukunja hadi kiganja cha mkono wa upande unaotaka kupima kiwe nyuma ya kisogo. Kwa kutumia kiganja cha mkono mwingine papasa na kubonyeza sehemu zote za titi kwa mduara, tokea pembeni huku ukibonyeza taratibu kuelekea kwenye chuchu hadi karibu na ndani ya kwapa. Baada ya hapo papasa na kubonyesha ziwa upande wa chini. Angalia iwapo utahisi tezi au uvimbe wowote, ngozi kuwa ngumu au mabadiliko ya aina yoyote. Kama umelala nyoosha mkono na kuulaza ili nao ulale kwenye kitanda pia. Baada ya hapo papasa na kubonyeza taratibu ziwa upande wa juu halafu papasa au bonyeza ziwa kwa pembeni karibu na ndani ya kwapa. Baada ya hapo papasa na kubonyesa ziwa upande wa chini na chuchu pia. Jambo muhimu ni kuzingatia iwapo kuna mabadiliko ya ngozi juu ya ziwa,kama vile hali ya ngozi juu ya ziwa kubadilika kusiko kawaida, chuchu ya ziwa kama inainamia chini, kuwepo utando, kutoka majimaji au damu kwenye chuchu na pia titi kuvimba. Pia kujaa au ukubwa wa titi usio wa kawaida au uliozidi ghafla. Jambo lingine la kuzingatia ni wekundu, weusi au joto katika ziwa. Kuingia ndani ngozi au kubadilika na kuwa kama ngozi ya chungwa, kuwasha, maumivu au vipele kwenye ngozi ya ziwa na uvimbe hata kama hauna maumivu.
Iwapo utahisi mabadiliko hayo tuliyoyatajwa unatakiwa kwenda hospitali kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi au unapaswa kumueleza daktari husika. Kwa kawaida kansa ya matiti huthibitishwa na kipimo cha mammograph ambacho huonesha tumor na uvimbe wa ugonjwa huo. Hata hivyo kujipima kansa ya matiti husaidia kutambulika mapema ugonjwa huo na kuanza matibabu mapema.
Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 75 hadi 90 ya magonjwa ya saratani, yanaweza kuzuilika kwa kubadili tu muundo wa maisha na kufuata kanuni za ulaji vyakula bora na kujiepusha na vyakula hatari na mtindo wa maisha unaosababisha maradhi mbalimbali, ikiwemo saratani. Moja ya njia mojawapo ya kujiepusha na kansa ya matiti na saratani zote kwa ujumla ni kujiepusha kula sukari kwa wingi.
Utafiti wa kisayansi umeonesha kuwa aina zote za sukari ni hatari kwa afya na sukari hurutubisha saratani. Sukari aina ya 'fructose' ndiyo mbaya zaidi na inatakiwa kuepukwa kadiri iwezekanavyo, hasa kwa mgonjwa wa saratani.
Tunashamburiwa kula vyakula vyenye vitamin D ambayo inahitajika karibu katika kila seli mwilini na ni mpiganaji mahiri dhidi ya chembechembe za saratani mwilini. Hivyo, kama wewe ni mgonjwa wa saratani, kiwango chako cha Vitamin D mwilini kinatakiwa kisiwe chini ya ujazo wa 70ng/ml. Pia Unashauriwa kula kwa wingi vyakula na vidonge maalumu vinavyoongeza vitamin hiyo au food supplements kwa kimombo. Vilevile tunashauriwa kula vitamin A. Kuna ushahidi pia unaoonesha kwamba vitamin A ina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani ya matiti. Lakini inashauriwa kupata vitamin A kutokana katika vyakula badala ya vidonge. Vyakula vyenye kiwango kingi cha vitamin A ni pamoja na nyama, maini na mayai ya kuku hasa wa kienyeji, maziwa na jibini.
&&&&&&&&
Tafiti zinaonyesha kwamba, ingawa watu wa umri wote wako katika
hatari ya kupatwa na kansa ya matiti lakini ugonjwa huo unawapata zaidi
wanawake baada ya umri wa miaka 40 na kuendelea. Lakini hii haimaanishi
kwamba wanawake walio chini ya umri huo hawapaswi kujichunguza mara kwa
mara ugonjwa huo. Wataalamu huwashauri wasichana wawe na mazoea ya
kujichunguza matiti yao toka wakiwa wadogo na kuangalia iwapo kuna
mabadiliko yanayoweza kuashiria uwepo wa ugonjwa huo. Pia wanawake wote
wanashauriwa kujifanyia wenyewe uchunguzi wa kansa ya matiti kwa uchache
mara moja kwa mwezi. Wataalamu wanasema kuwa, asilimia 40 ya kesi za
ugonjwa wa kansa ya matiti hugunduliwa na wanawake kwa huhisi uvimbe,
hivyo mazoea ya kujifanyia uchunguzi ili kuangalia kama wamepatwa na
ugonjwa huo ni jambo muhimu sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba
kipimo cha mammography kinaweza kumsaidia mwanamke kugundua kensa kabla
ya kufanya uvimbe, lakini kujichunguza mwenyewe kunamsaidia mwanamke
kuwajuza mapema wataalamu wa afya iwapo ataona mabadiliko yoyote
yanayoweza kusababishwa na kansa ya matiti. Tunashauriwa kuwa, muda bora
wa kufanya breast self examination ni siku 3 hadi 5 baada ya kuanza
hedhi. Namna ya kujichunguza matiti au breast self exam ni kama
ifuatavyo. Kwanza kabisa ni vizuri zaidi uchunguzi huo ukifanywa wakati
mtu akiwa amelala kwenye kitanda au akiwa mbele ya kioo kinachoweza
kuonesha vizuri kiwiliwili hasa upande wa juu. Kama umesimama nyoosha
mkono wako na kuukunja hadi kiganja cha mkono wa upande unaotaka kupima
kiwe nyuma ya kisogo. Kwa kutumia kiganja cha mkono mwingine papasa na
kubonyeza sehemu zote za titi kwa mduara, tokea pembeni huku ukibonyeza
taratibu kuelekea kwenye chuchu hadi karibu na ndani ya kwapa. Baada ya
hapo papasa na kubonyesha ziwa upande wa chini. Angalia iwapo utahisi
tezi au uvimbe wowote, ngozi kuwa ngumu au mabadiliko ya aina yoyote.
Kama umelala nyoosha mkono na kuulaza ili nao ulale kwenye kitanda pia.
Baada ya hapo papasa na kubonyeza taratibu ziwa upande wa juu halafu
papasa au bonyeza ziwa kwa pembeni karibu na ndani ya kwapa. Baada ya
hapo papasa na kubonyesa ziwa upande wa chini na chuchu pia.Iwapo utahisi mabadiliko hayo tuliyoyatajwa unatakiwa kwenda hospitali kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi au unapaswa kumueleza daktari husika. Kwa kawaida kansa ya matiti huthibitishwa na kipimo cha mammograph ambacho huonesha tumor na uvimbe wa ugonjwa huo. Hata hivyo kujipima kansa ya matiti husaidia kutambulika mapema ugonjwa huo na kuanza matibabu mapema.
Utafiti wa kisayansi umeonesha kuwa aina zote za sukari ni hatari kwa afya na sukari hurutubisha saratani. Sukari aina ya 'fructose' ndiyo mbaya zaidi na inatakiwa kuepukwa kadiri iwezekanavyo, hasa kwa mgonjwa wa saratani.
Tunashamburiwa kula vyakula vyenye vitamin D ambayo inahitajika karibu katika kila seli mwilini na ni mpiganaji mahiri dhidi ya chembechembe za saratani mwilini. Hivyo, kama wewe ni mgonjwa wa saratani, kiwango chako cha Vitamin D mwilini kinatakiwa kisiwe chini ya ujazo wa 70ng/ml. Pia Unashauriwa kula kwa wingi vyakula na vidonge maalumu vinavyoongeza vitamin hiyo au food supplements kwa kimombo. Vilevile tunashauriwa kula vitamin A. Kuna ushahidi pia unaoonesha kwamba vitamin A ina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani ya matiti. Lakini inashauriwa kupata vitamin A kutokana katika vyakula badala ya vidonge. Vyakula vyenye kiwango kingi cha vitamin A ni pamoja na nyama, maini na mayai ya kuku hasa wa kienyeji, maziwa na jibini.
No comments:
Post a Comment