Wanasayansi wanasema kuwa wanawake ambao hula chips au 'crips' kila siku
wanaweza kuongeza mara mbili hatari ya kensa ya kizazi na ya ovari.
Hatari hiyo inatokana na mada iitwayo acrylamide, ambayo hupatikana
wakati wa kukaanga, kuoka au kuchoma vyakula mbalimbali. Wataalamu wa
Kidachi wamewafanyia uchunguzi watu 120,000 juu ya tabia yao ya ulaji na
kugundua kuwa wanawake ambao wanakula vyakula vyenye acrylamide,
wanaonekana kukabiliwa na hatari zaidi ya kupatwa na aina hizo za
saratani.
Vyakula ambavyo vinapata rangi mbalimbali au kuungua wakati wa
kupikwa vinaonekana kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na
acrylamide. Wataalamu wa vyakula wanasema kuwa, ni wazi kuwa haiwezekani
kuondoa aina hizo za vyakula moja kwa moja katika lishe yetu. Uchunguzi
kuhusiana na masuala hayo umeonyesha kuwa, wale ambao wanakula
mikrogram 40 za acrylamide kwa siku ambayo ni sawa na nusu ya pakiti ya
biskuti, sahani ya chipsi ya paketi moja ya crisp, basi wanakabiliwa na
hatari ya kupatwa na kensa mara mbili zaidi ikilinganishwa na wale
wanaokula acrylamide kwa kiasi kidogo zaidi ya hicho. Hata hivyo
wataalamu wa uchunguzi huo wanawatoa shaka watu kwa kusema kuwa, matokeo
ya uchunguzi huo yanapaswa kuthibitishwa zaidi na uchunguzi mwingine.
No comments:
Post a Comment