Je, ni vipi hushambulia ngozi?
Maeneo yenye mabaka yanayoletwa na fangasi wa aina hii hubadilika rangi yake na kuwa na rangi hafifu au inayoonekana zaidi (kama ni mtu mwenye rangi ya maji ya kunde basi ngozi iliyoathiriwa hubadilika na kuwa nyeupe au nyeusi sana.
Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.
Upungufu huo ya rangi ya ngozi si wa kudumu, bali ngozi hurudi kwenye hali ya kawaida ya rangi yake baada ya muda mrefu kidogo tangu maradhi halisi yalipokomeshwa. Bila matibabu maradhi haya huchukua muda kupona hivyo dawa ni muhimu ili mwenye maradhi aweze kupona upesi.
Namna ya kuyatambua
Maradhi haya ni rahisi kuyagundua ila kutokana na kufanana kwake na maradhi mengine yenye dalili kama hizi uhakiki wa vimelea vinavyosababisha maradhi haya ni muhimu.
Sehemu ya ngozi kutoka kwenye eneo lenye maambukizi huchukuliwa na kupelekwa maabara ambako sehemu hii ya ngozi huwekwa kwenye darubini maalum kwa ajili ya kuangalia vimelea hivi vya fangasi.
Nini matibabu yake?
Maradhi haya huweza kutibika kirahisi, ila mara nyingi hurudia kushambulia ngozi hasa eneo ambalo liliwahi kushambuliwa kabla.
Kutokana na uwezo wake wa kurudia kuambukiza ngozi huwa inashauriwa kwa aliyewahi kupata maradhi haya kurudia kutumia dawa ya kuua vimelea vya fangasi mara kwa mara ili kuondoa uwezekano wowote wa maradhi kurudia kushambulia.
Matibabu ya maradhi haya huhusisha dawa za kupaka zinazoua vimelea hivi vya fangasi
Dawa za kuua vimelea vya fangasi za kunywa pia hutolewa kwa ajili ya kutibu aina hii ya fangasi lakini hushauriwa zitolewe tu kama dawa za kupaka zimeshindwa kuua vimelea hivi vya fangasi.
Maradhi yanayofana nayo:
Kuna magonjwa ambayo hufanana na maradhi haya. Mfano ;
-Pumu ya ngozi
-Vitiligo
Maradhi haya tutayazungumzia kwenye makala zijazo kwenye mtiririko huu.
Matokeo baada ya matibabu
Kama nilivyoandika hapo juu maeneo ya ngozi yaliyobadilika rangi huweza kubaki hivyo hata baada ya vimelea vya fangasi kuondolewa na dawa.
Hii inamaanisha inawezekana kabisa mgonjwa akabaki na mabaka yanayotokana na vimelea hivi vya fangasi muda mrefu hata baada ya kutumia dawa ambayo imefanikiwa kuondoa vimelea hivi vya fangasi. Hali hii mara nyingi huchanganya wagonjwa na kusababisha wagonjwa kudhani kuwa maradhi bado upo hivyo kuendelea kutumia dawa au kuanza kutumia dawa baada ya muda mfupi tangu kumaliza kutumia dawa zilizofanikisha uondoaji wa vimelea.
Hali ya sehemu ya ngozi iliyoathiriwa na vimelea vya fangasi kurudisha rangi ya kawaida ya ngozi kama sehemu nyingine ambazo hazikua na madhara huchukua muda mrefu kidogo ingawa kama eneo husika lilikua na uvimbe basi uvimbe hupotea haraka.
IMETOKA KWA:
DR ISAAC MARO
No comments:
Post a Comment