KUVIMBA kwa kuta za uke kutokana na kushambuliwa na fangasi (candida
albicans ) au bakteria. Kuta hizi huanza kuwa na vijitundu vidogo vidogo
na kadiri muda unavyokwenda bila kutibiwa vitundu hivi huongezeka
ukubwa na kuwa kama vidonda na hatimaye kuta za uke kuanza kumomonyoka
na hali hii huondoa kabisa hamu ya kushiriki tendo.
Matatizo ya shingo ya kizazi (cervical incompetence) kutokana na
maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi
au masaa kadhaa baada ya tendo ni dalili kuu ya tatizo hili. Pia
mwanaume anapogonga shingo hii ya kizazi mwanamke huwa kama anatoneshwa
kidonda. Hali hii ya mbegu kurudi nje husababisha mwanamke kutoshika
ujauzito.
Kuwa na uvimbe kwenye mji wa mimba/mfuko wa uzazi( Uterus). Uvimbe
huu kitaalam hujulikana kwa majina mengi lakini `fibroid` ni maarufu
zaidi. Huanza kama mbegu ndogo ya mchicha na hukua kubwa kama boga
kubwa. Mwanamke huongezeka ukubwa wa tumbo na baadae huonekana kama ana
mimba kubwa na watu hushangaa kwa nini hajifungui kipindi chote.
Maumivu wakati wa tendo hasa chini ya kitovu huashiria tatizo kwenye
mirija ya uzazi. Yawezekana ikawa ni tatizo la mirija ya uzazi kujaa
maji machafu kutokana na kuzaliana sana eneo hilo, tatizo ambalo
hujulikana kitaalamu kama Hyrosalpinx.
Kitu hiki husababisha mirija ya uzazi kuziba kwani maji haya huwa
mazito, kitu ambacho hupelekea mayai ya uzazi na mbegu za kiume
kushindwa kupenya. Kutoshika mimba kwa mwanamke aliye kwenye ndoa au
mahusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja na anasikia maumivu ya aina hii ni
kiashiria kikubwa cha tatizo hili.Pia kuna tatizo la kuvimba kwa kuta za
mirija ya uzazi yaani Salpingitis. Hili pia husababisha mirija kuziba
kama lisipotibiwa mapema. Vyanzo vya tatizo hili tutajifunza siku
zijazo.
Maumivu wakati wa tendo chini ya kitovu pia huashiria tatizo la
mwanamke kuwa na mrundikano wa vijivimbe vingi kwenye vifuko vya mayai
ya uzazi.Kitaalam linaitwa Polysystic Ovarian Syndrome (PCOS )au Stain
Livingthal Syndrome.
Kama mwanamke anasikia maumivu haya na wakati huo huo anaona siku
zake za hedhi zinapishanapishana sana, na pia kuona uchafu kama maziwa
mtindi unatoka ni dalili kubwa ya tatizo hili na hasa kama anaviashiria
vya kuwa na homoni nyingi za kiume mfano kuwa na ndevu au vinyweleo
vingi mikononi na miguuni.
No comments:
Post a Comment