Harufu mbaya ya mdomo husababishwa na kutofanya usafi pamoja na maambukizi sehemu mbalimbali za mdomoni au kwenye njia ya hewa Ili huweze kupunguza na kuzuia hali hiyo fanya yafuatayo:
- Fanya usafi wa mdomo na kunywa maji mengi mara kwa mara
- Kila baada ya chakula weka maji mdomoni na sukutua kwa muda wa sekunde kadhaa ili kuondoa mabaki ya chakula.
- Baada ya kula unaweza kutafna mchanganyiko wa mbegu za iliki na karafuu ambazo husaidia kupunguza harufu mbaya mdomoni
- Pia unaweza kusuuza mdomo kwa kutumia mchanganyiko Mdalasini, iliki na karafuu kuua vijidudu na vimelea mbalimbali mdomoni na katika njia ya hewa
- Pia unaweza kusafisha mdomo kwa Juice ya limao kwani huzuia kukua na kuenea kwa bakteria na fungasi
- Kama umefanya yafuatayo na bado tatizo linaendelea muone dakitari kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment