Watafiti wametoa tahadhari kuwa vijidudu vya malaria
visivyoweza kuuawa kwa dawa vimetapakaa katika maeneo ya mpakani kusini
mashariki mwa Asia vikitishia mapambano dhidi ya Malaria.
Vipimo kwa wagonjwa 1000 katika maeneo ya
Cambodia, Burma, Thailand na Vietnam vimegundua vijidudu hivyo
havizuiliwi na artemisinin dawa inayoaminika katika vita dhidi ya
malaria. Utafiti huo umeeleza kuwa kuyarudiaThursday, 31 July 2014
VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA
PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au kamasi kutoka. Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mgusu wa hisia za raha. Pia pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kumshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) na pia ili ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa uweze kupata hisia kila sehemu
Monday, 28 July 2014
TAMBUA MAPEMA KAMA UNA TATIZO LA SARATANI YA MATITI
Saratani ya matiti ni ya pili kwa ukubwa na mara nyingi
huwapata zaidi wanawake hasa wenye umri zaidi ya miaka 50. Kama unahisi uvimbe wowote au mabadiliko
yoyote yasiyo ya kawaida katika maziwa unatakiwa kuwahi mapema hospitali kwa
uchunguzi kabla tatzo halijawa sugu. Saratani hii hutibiwa mapema katika hatua
za awali kabla haijasambaa katika maeneo mengine ya mwili kupitia mirija, tezi
na mishipa ya damu. Ikumbukwe kuwa
wanawake huweza kuhisi uvimbe, maumivu na maziwa kujaa na kuwa makubwa hasa
kipindi cha hedhi na ujauzito hivyo ni
muhimu kutofautisha hali hii ambayo ni ya kawaida na saratani ya maziwa.
MBEGU ZA MABOGA ZINA UWEZO WA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 10 HATARI
Zikiwa zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa,
maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na
muhimu kutafuna kila wakati kama wewe ni mpenzi wa kutafuna-tafuna.
Imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki
kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10:
Thursday, 17 July 2014
MADHARA YA VIPODOZI NA PAFYUME
Vipodozi ni mojawapo ya vitu ambavyo humfanya mtu avutie na kubadili na kuongeza mwonekano, umbo na harufu ya binadamu. Hii inaweza kujumuisha cream, losheni, poda, pafyuma, body spray, waves, mafuta ya kuogea, deodoranti, kucha na kope za kubandika, lipsticks na lipshine, shampoo na vipodozi vya aina mbali mbali. Pamoja na kuongeza mvuto wa ngozi na mwili vipodozi huweza kusababisha madhara yafuatayo:
Magonjwa ya ngozi hili ni tatizo sugu kwa watumiaji hasa wa muda mrefu wa vipodozi kwani husababisha kuungua. kuvimba, kuharibika na kutoka vipele kwenye ngozi ambayo huchukua muda mrefu kutibika au kutotibika kabisa.
Muwasho na Allergy hii huweza kuathiri ngozi, maskio, tumbo na mifumo wa upumuji na fahamu kutokana na harufu kali au kemikali zilizopo katika vipodozi hivyo kumpasa mtumiaji kuwa makini na uchaguzi wa vipodozi.
Magonjwa ya ngozi hili ni tatizo sugu kwa watumiaji hasa wa muda mrefu wa vipodozi kwani husababisha kuungua. kuvimba, kuharibika na kutoka vipele kwenye ngozi ambayo huchukua muda mrefu kutibika au kutotibika kabisa.
Muwasho na Allergy hii huweza kuathiri ngozi, maskio, tumbo na mifumo wa upumuji na fahamu kutokana na harufu kali au kemikali zilizopo katika vipodozi hivyo kumpasa mtumiaji kuwa makini na uchaguzi wa vipodozi.
Wednesday, 16 July 2014
HABARI NJEMA KATIKA VITA DHIDI YA UKIMWI
Kuna uwezekano kuwa janga la ukimwi huenda
likadhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kulingana na ripoti iliyotolewa na
shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi.
Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya visa vya maambukizi mapya na vifo kutokana na HIV, vimeendelea kushuka.
Hata hivyo, shirika hilo linataka juhudi zaidi za kimataifa kufanywa kwani za sasa hazitoshi
Na shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 35 wanaishi na virusi vya HIV.
Ripoti hiyo ilionyesha visa vipya vya maambukizi milioni 2.1 vilitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001.
Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.
Afrika Kusini na Ethiopia zimepiga hatua katika kupunguza vifo vya wagonjwa wa HIV
.IMETOKA http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/07/140716_hiv_unaids.shtml
Monday, 14 July 2014
JE WAJUA?: UYOGA NI KINGA YA MAGONJWA
Uyoga hufanya damu kuwa nyepesi, unazuia saratani, unashusha kiwango cha kolestro, huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili na hudhoofisha virusi
Wednesday, 9 July 2014
Ugonjwa wa Mtoto Jichoni (Cataracts)
Mtoto jichoni ni nini?
Huku ni kuwa na mawingu kewnye kioo asili cha jicho (natural lens)
kioo hiki ndicho hukuwezesha kuelekeza mishale ya nuru ili kutoa sura
ilizo dhahiri. Huweza kutokea katika jicho moja au yote na husambaa kutoka jicho moja hadi lingine.
Baadhi ya mambo yanayosababisha mtoto jichoni ni:
TATIZO LA UVIMBE KATIKA KIZAZI KWA WANAWAKE
Tatizo hili la uvimbe ambao sio saratani huwatesa wakina
mama na wasichana wengi na hivyo kufikia hatua ya kuondolewa kizazi endapo
hautowaiwa na kutibiwa katika dalili za awali. Ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa fibroids au
leimyoma na huathiri zaidi ya asilimia 25 ya wanawake wa kiafrica na asilimia 50
ya wazungu. Uvimbe huu huwa katika umbile la misuli laini na myembamba na hukua
siku hadi siku kutokana na vichocheo vya estrogeni hasa kipindi cha hedhi na
ujauzito.
Uvimbe huu hujitokeza
katika ukuta wa kati, wa nje, au ndani kabisa ya nyumba ya uzazi na huambatana
na dalili zifuatazo.
Subscribe to:
Posts (Atom)