Friday, 11 September 2015

HIZI NI DALILI ZA AWALI ZA UGONJWA WA KISUKARI, ZITAMBUE NA EPUKA MAPEMA UGONJWA HUU HATARI.

Zaidi ya robo tatu ya wagonjwa wa kisukari huwa na dalili na ishara  ambazo hushindwa kuzitambua mapema hivyo kukosa vipimo na matibabu ya mapema kukabiliana na tatzo hili. Zifuatazo ni ishara na dalili za awali zitakazokusaidia kujua kama unakabiliwa au uko katika hatari ya ugonjwa wa kisukari.

  1. Kukojoa mara kwa mara.
  2. kupata kiu na njaa mara kwa mara au kwa muda mrefu.
  3. Midomo kuwa mikavu.
  4. Kupungua uzito au kuongezeka uzito kwa kasi,
  5. Kupoteza nguvu na uchovu wa mara kwa mara au muda mrefu
  6. Maumivu ya kichwa.
  7. Miguu na mikono kufa ganzi
  8. Kutokuona vizuri au kuona mawenge. 

Endapo unasumbuliwa zaidi na mojawapo kati ya dalili hizi na unahisi una ugonjwa huu ni muhimu kuwahi hospitali au vituo vya afya kwa ajiri ya matibabu yanayohusisha lishe, dawa na mazoezi ili kuepuka madhara ,makubwa ya ugonjwa huu.

 
BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WAELIMISHE MARAFIKI

No comments:

Post a Comment

.