Friday, 11 September 2015

SOMA KUHUSU UFADHILI MPYA WA UTAFITI BARANI AFRIKA

Hazina mpya ya kufadhili utafiti wa kisayansi imeanzishwa barani Afrika, huku kukiwa na wasi wasi kuwa utafiti unaofanyika barani kwa kiasi kikubwa hufanywa na watu kutoka Mataifa ya Magharibi.
Wafadhili wa mradi huo unaojulikana kama Muungano wa Kuimarisha Sayansi barani Afrika, Alliance for Accelerating Excellence in Science in Africa, (AESA), wanasema ukosefu wa uwekezaji katika secta ya Sayansi umehujumu maendeleo barani.

Shirika hilo la EASA limesema litatoa dola milioni mia moja kwa utafiti utakaohusisha bara la Afrika.
Inatarajiwa kuwa serikali za mataifa ya Afrika yatawekeza asilimia moja ya mapato yake ya mwaka wa utafiti wa sayansi.
Shirika hilo lilibuniwa na Chuo cha mafunzo ya Sayansi barani Afrika, huku ikifadhiliwa na kampuni ya Welcome Trust, Wakfu wa Gates na serikali ya Uingereza.
Rais wa Mauritania, Ameenah Gurib-Fakim, ameiambia BBC, kuwa dhamira kuu ya utafiti unaofadhiliwa kutoka nje ya bara la Afrika, mara nyingi huazingatia au kutatua masuala yanayohusu bara hili.
Amesema hatma ya Afrika siku Zijazo, itategemea ikiwa utafiti wa sayansi utaimarishwa.
Shirika la AESA, litaanza kufadhili miradi ya watafiti saba barani afrika.
Watafiti hao ni pamoja na Dixon Chibanda kutoka Zimbabwe anayefanya utafiti kuhusu ukosefu wa matibabu ya kiakili nchini humo, Thumbi Ndungu wa Afrika Kuisni ambaye anafanya utafiti kuhusu jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu na Ukimwei barani Afrika.
Watafiti wengine kutoka Ghana, Mali, Uganda na Kenya watafadhiliwa.

No comments:

Post a Comment

.