Matumizi ya dawa za kurefusha maisha (ARVs) kwa waonjwa wa Ukimwi ni changamoto na wagonjwa wengi huchelewa kujigundua na kuanzisha dawa mapema ili kuongeza na kuzuia kushuka kwa CD4 ambazo humkinga mgonjwa na maambukizi na magonjwa nyemelezi ambayo udhoofisha afya ya mgonjwa na kusababisha vifo.
Tafiti zinaonyesha kuwa wagonjwa wanaojitambua mapema na kuanzishiwa dawa hupata faida na matokeo mazuri sambamba na kujinga na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na magonjwa ya zinaa.
No comments:
Post a Comment