Thursday, 28 May 2015

TAHADHARI JUU YA MATUMIZI YA DAWA ZA PARACETAMOL

Wanawake wajawazito wanapaswa kutahadhari zaidi wanapotumia dawa zozote zilizo na chembechembe za Paracetamol.
Utafiti wa Wanasayansi nchini Uingereza umebaini kuwa unywaji wa dawa zenye kiungo cha Paracetamol kwa kipindi cha siku saba unapunguza uwezo wa uzalishaji wa homoni za kiume ''testosterone''.

Homoni hiyo ''testosterone'' ndio inayowezesha kuumbwa kwa sehemu ya uzazi wa kiume .
Sasa madaktari wanashauriwa wasipeane dawa zenye ''Paracetamol'' kwa wanawake waja wazito kiholela.
Na iwapo itawalazimu kupeana dawa hizo basi wanashauriwa kupeana dawa hizo kwa kipindi kifupi ilikupunguza madhara kwa watoto waliotumboni.
Halmashauri inayosimamia matumizi ya madawa nchini Uingereza sasa inasema licha ya kuwa inahujumu kiumbe kilichoko tumboni, Paracetamol ni moja kati ya madawa yenye madhara machache zaidi kwa mama mja mzito na mwanawe.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa onyo kutolewa dhidi ya wanawake wajawazito kupewa dawa zilizo na kiuongo cha Paracetamol.
Awali utafiti wa wanawake waja wazito 2,000, nchini Denmark ulibaini kuwa,wanawake waliomeza dawa za Paracetamol walijifungua watoto waliolemaa katika sehemu ya mfuko wa uzazi- korodani.
Ulemavu huo hatimaye ulijitokeza na kuwa upungufu wa uwezo wao kuzalisha katika maisha yao ya utu uzima.
Paracetamol yaathiri uwezo wa kuzalisha:Utafiti
Aidha inasemekana kuwa wanawake wanaotumia dawa hiyo ya kupunguza maumivu kwa kipindi kirefu wakati wa ujauzito, wanaweza kuathiri mimba zao na hasa kwa watoto mvulana.
Wanasayansi hao wa Chuo kikuu cha Edinburgh, walitumia panya katika utafiti huo.
Shirika linalosimamia maswala ya afya Nchini Uingereza, linasema kuwa wanawake waja wazito wanafaa kumeza tembe hiyo ya paracetamol ikiwa tu wameshauriwa na daktari na pia kwa kipindi kifupi mno.
Dakta Dr Rod Mitchell, aliyeongza utafiti huo anasema kuwa tahadhari kubwa inapaswa kuwekwa inapowadia swala la matumizi ya Paracetamol miongoni mwa wanawake waja wazito.
''utafiti huu unatilia pondo ushauri tuliokuwa nao tayari kuwa chembechembe za dawa hiyo zinaathiri ukuawaji wa sehemu za kiume za watoto wavulana''
Utafiti huo ulifaulu baada ya madaktari kuwapasua panya na kuwapandikiza mimba na kisha wakawapa dawa hiyo kwa siku saba.
Walipoipima iwapo ilikuwa na chembechembe za homoni hiyo ya kiume waligundua kuwa haikuwa nayo.
Hata hivyo walipoipima baada ya siku moja hawakuona tofauti ya viwango ya homoni hiyo muhimu kwa wanaume.
CHANZO BBC 

No comments:

Post a Comment

.