1. Boresha Lishe
Chakula ni chanzo kikubwa cha afya. Lakini pia chakula ni chanzo kikubwa cha magonjwa kwa wengi wetu. Utamaduni wako wa kula hukufanya uzidi kunawiri au kuharibu mwili. Hivyo, kuwa makini na chakula chako. Kama tunavyosisitiza, pendelea kula mboga za majani, vyakula vilivyo na virutubisho asilia na kunywa maji kwa wingi.2. Punguza Ulevi
Maisha si rahisi, hii si ajabu. Lakini kigezo cha ugumu wa maisha isiwe sababu ya kutumbukia kwenye tabia za kulewa na kutumia vitu vingine vya kujiliwaza. Pombe ni hatari kama ikinywewa kupitiliza. Sigara vilevile ni hatari ikitumiwa kwa muda mrefu.Ni vizuri mwaka huu tuwe na lengo la kupunguza kuvuta sigara na kunywa pombe. Hii itatusaidia kuongeza muda kufanya vitu vingine muhimu badala ya kukaa kwenye vikao vya pombe kila jioni. Ikishindikana kabisa kuacha basi tuwe tuna muda maalumu wa siku moja au mbili wakati wa weekend ili kuweza kutumia muda wa wiki kwa shughuli za maendeleo.
3. Fanya Zoezi
Hili halina haja ya msisitizo zaidi. Watu wengi wanapenda kufanya mazoezi ili kupunguza uzito. Lakini mazoezi maana yake siyo tu kupunguza uzito. Mazoezi yana kazi kubwa ya kuufanya mwili kufanya kazi vizuri, kuongeza mzunguko wa damu mwilini na kuleta mzunguko mzuri wa hewa kwenye mapafu na vilevile kuufanya mwili kuwa imara dhidi ya magonjwa. Swala la kupungua uzito ni muhimu lakini ni ziada. Haimaniishi kama una umbo linalofaa basi usifanye mazoezi, hapana. Mazoezi ni muhimu kwa mtu yeyote ili kuufanya mwili uwe katika afya njema.Weka lengo la kufanya mazoezi mara mbili au tatu kwa wiki. Hii inatosha kuanza ili kuweza kuweka mwili kwenye hali nzuri. Afya siyo kitu cha siku moja, bali ni swala la kila siku.
4. Funga Kula na kunywa
Afya siyo kula tu. Afya pia hutegemea kujinyima. Vyakula vingi tunavyokula hutuletea sumu na vitu vingi ambavyo vinadhuru miili yetu. Tukipata muda wa kufunga na kujinyima kula vyakula, mwili hupata nafasi ya kuondoa uchafu, kujisafisha na kuwa na afya bora. Hivyo, ni vizuri kuwa na muda wa kufunga kila mara ili kuweza kuboresha afya.5. Mapumziko
Afya inahusisha vitu vingi, lakini kupumzika ni kitu muhimu sana. Ni ukweli kuwa unaweza kukaa bila kula kwa siku nyingi zaidi mfululizo kuliko kukaa bila kulala. Kutopumzika vizuri kunapunguza ufanisi wako kwenye mambo yako ya maendeleo. Kukosa sana usingizi kunasababisha kupata magonjwa makubwa zaidi ya kiakili na kisaikolojia. Hivyo kushindwa kufikia malengo yako.Kupumzika n
i muhimu, maana ndio chanzo kikubwa cha ufanisi kwenye shughuli zako za kila siku. Jaribu kulala masaa 7 hadi 8 kwa siku. Huu ndio muda ulio muafaka ili kuufanya ubongo wako uweze kufanya kazi kwa ufasa zaidi.
6. Boresha Mahusiano
Mahusiano yako ni kigezo kimoja kikubwa sana cha afya yako. Watu wenye afya bora huwa na mahusiano bora. Ukiwa unapenda maendeleo na una malengo ya kufika mbali, lazima uwe unajiheshimu ukiwa na mwenzi wako.Ni vizuri kujiepusha na magonjwa ili uweze kufaidi maisha. Kuwa na mahusiano yasiyo ya afya na watu wengi Zaidi huongeza uwezekano wa maambukizi ya magojwa ya zinaa. Hivyo kukupunguzia muda wa kufanya mambo yako muhimu maishan
No comments:
Post a Comment