Friday, 28 August 2015

KAMA UNASUMBULIWA NA FANGASI SEHEMU ZA SIRI

Candida albicanas ni aina ya fangas wanaoweza kuathiri sehemu mbalimbali ya mwili wa binadamu. Mara nyingi hushambulia sehemu laini za mwili (mucuos membrane), pia wanaweza kuathiri ngozi na kusambaa kwenye damu hasa kwa wagonjwa wenyewe upungufu wa kinga.


Zaidi ya asilimia 78 ya wanawake hupata maambukizi ya  fungus sehemu za siri mara moja au zaidi katika maisha. Hata hivyo baadhi hupata maambukizi  mara kwa mara.Maambukizi hufanya na aina ya fangas waitwa Candida albicans. Fangasi hawa kwa kawaida hupatika katika njia ya uzazi ya mwanamke bila madhara yoyote, lakini  mabadiliko ya hormoni na upungufu wa kingi mwilini sambamba na maambukizi mbalimbali huweza kusababisha ugonjwa. 



DALILI
Ugonjwa huu unaweza kuwa na dalili mbalimbali 
Mgonjwa anaweza kusikia miwasho, kuchubuka sehemu za siri, kusikia maumivu wakati wa kujamiiana au wakati wa kukojoa na pia kutoa uchafu mweupe kama maziwa mgando ambao kwa kawaida hauna harufu.
Pi dalili hizo zinaweza kuambatana   na kuvimba mashavu ya njia ya uzazi, kidonda au mipasuko.

MATIBABU
Dawa za aina tofauti kama  clotrimazole  miconazole fluconazole nystatin na fluconazole zinaweza kutumika kutibu ugonjwa huu  kwa muda wa siku 5 mpaka 14 kutokana na ukubwa wa tatizo.. Dawa zinaweza kuwa za kutumbukiza kwenye njia ya uzazi wa mwanamke, kupaka(cream) na wakati mwingine mgonjwa anaweza kuandikiwa dawa za kumeza iwapo amekuwa akipata ugonjwa huu mara kwa mara.
Pia epuka kuvaa ngua za kubana na kuacha unyevunyevu sehemu za siri sambamba na kufanya usafi mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

.