Masaji ni tiba mojawapo inayoweza kukusaidia kupunguza
uchovu, maumivu, kupumzisha akili na kurekebisha mzunguko wa damu. Zifuatazo ni aina za masaji
ambazo unaweza kufanya ili kuweka mwili wako katika hali nzuri
Masaji ya kutumia jiwe( Hot stone massage)
Hii ni aina ya masaji ambayo hufanywa kwa kutumia mawe laini
na yenye joto kiasi kulainisha misuli na kupunguza maumivu kwa kuifanya misuli
isinyae na kulegea
.
Masaji ya kutumia mafuta (Aromatherapy massage)
Masji hii ni maarufu na hutumika mara nyingi kwa kutumia
mafuta maalumu(Aroma oil) na hupoza na kutuliza mwili uliochoka pia hupunguza
mawazo na kutuliza akili, pia mafuta aina lavender na Rose au aina nyingine
tofauti huweza kutumika kutokana na upatikanaji wake katika maeneo husika
Masaji katika tishu za ndani (Deep tissue Massage)
Hii hufanywa kwa nguvu ili kufikia tishu na misuli ya ndani
kwa ajili ya kuondoa maumivu ya muda mrefu yanayosababishwa na magonjwa mbali
mbali ya mifupa na misuli. Pia huweza kusaidia kuondoa makovu yatokanayo na
kuumia kwa sehemu za ndani za mwili
Masaji ya miguu (Foot massage)
Hii hufanywa kwa kutumia ncha za vidole au kipande kidogo
cha ubao kinachotumika kuweka pasha na kulainisha sehemu za miguu kuanzia
unyayo mpaka kwenye magoti na kiunoni na mara nyingi huwa ni kwa ajili ya
kupumzika na kujifurahisha ila huweza kuondoa maumivu kwa mama mjamzito anapokaria
kujifungua na kupunguza mawazo.
Masaji ya mgongoni (Back massage)
Hii hufanywa kulainisha misuli na viungo katika sehemu ya
mgongo ili kupumuzisha mwili na kusaidia mzunguko mzuri wa damu katika mabega
na shingo. Hii pia ni rahisi kuliko zote kwani huweza kufanywa nyumbani bila
maelekezo yoyote ya kitaalamu ukilinganisha na nyingine.
Masaji kwa wajawazito (Pregnancy massage)
Hii hufanywa na wataalamu wa afya kuondoa na kupunguza
mawazo, maumivu na uvimbe huku akiwekwa katika mkao mzuri kuzuia madhara kwa motto.
Hata hivyo inashauriwa kutokufanya
masaji hii kipindi cha miezi mitatu ya ujauzito na wale wenye matatizo ya
kiafya.
KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA
HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI
No comments:
Post a Comment