Friday, 9 May 2014

MAELEZO KUHUSU UGONJWA HATARI WA DENGUE NCHINI

Dengu ni ugonjwa wa mlipuko unaosababishwa na virusi vinavoenezwa na mbu aina ya Aedes aegypti wanaouma muda wowote
kuna aina mbili za ugonjwa huu ugonjwa wa papo kwa papo (Acute)  ambao huchukua muda wa wiki moja mpaka mbili na ugonjwa wa muda mrefu(chronic) baada ya wiki mbili na kuendelea.

DALILI ZA AWALI
Dalili za ugonjwa huu ufanana sana na magonjwa ya malaria na mafua hivyo ni muhimu kuwahi hospitali zenye vipimo ili kutambua ugonjwa huu uonapo dalili hizi:
  • Maumivu sehemu za jointi na misuli
  • Kuvimba kwa tezi mbalimbali za mwili
  • maumivu ya kichwa na nyuma ya macho
  • Vipele katika sehemu za ngozi pamoja na homa kali
  • kichefuchefu na kutapika

DALILI ZA BAADAE
Endapo ugonjwa huu hautotibika mapema huweza kupelekea dalili za awali kuwa kali sana na kuingia katika hatua ya Dengue hemorrhagic fever (DHF) sambamba na maumivu makali ya tumbo kupumua kwa kasi, mwili kuchoka na kutapika damu, mshtuko na kukosa fahamu hatimaye kusababisha kifo.


MATIBABU
Kutokana na ugonjwa huu kusababishwa na virusi hakuna matibabu kamili kwa ugonjwa huu zaidi ya kutibu na kuondoa dalili za ugonjwa huu mapema ili kuzuia vifo. Maumivu, uvimbe na homa huweza kupunguzwa kwa kutumia dawa zozote rahisi za kutuliza maumivu kama paracetamol. Wakati dalili za mafua huweza kutibiwa na kutulizwa kwa dawa yoyote ya kutibu mafua na kunywa maji mengi.

Mgonjwa aliye katika hatua ya Dengue hemorrhagic fever (DHF) huitaji kulazwa hosipali kwa muda ambapo dripu za maji, chakula na dawa huitajika ili kuokoa maisha yake.

JINSI YA KUZUI MAAMBUKIZI
Kufanya usafi na kuondoa mazali ya mbu
kuvaa  ndefu na zisizobana hili kuepuka kuumwa na mbu
kufanya usafi wa nyumba na kupuulizia dawa ya mbu walau kila baada ya wiki moja
kulala ndani ya chandarua chenye dawa ya kuua mbu
KWA MSAADA ZAIDI BOFYA HAPA AU ACHA COMMENT CHINI

No comments:

Post a Comment

.