Ili kuepuka ghalama na usumbufu unaosababishwa na ugonjwa huu unaweza kuzingatia mambo yafuatayo ili huweze kujikinga na kuzuia ugonjwa huu.
- Kunywa maji mengi kiasi cha glasi 6 mpaka 8 itakusaidia kukojoa mara kwa mara na hupunguza idadi ya maambukizi katika njia ya mkojo
- Epuka vyakula na vinywaji vinavyoweza kukuweka katika hatari ya maambukizi, kama kahawa na pombe ambavyo hupunguza kinga za mwili.
- Safisha njia ya mkojo(Urethra) kila baada ya kukojoa na kufanya tendo la ndoa kuanzia mbele kuelekea nyuma ili kuepuka wadudu katika njia ya haja kubwa kuingia katika njia ya mkojo
- Epuka dawa na poda zinazopuliziwa katika njia ya haja ndogo au kuingiza vitu au vidole pasipostahili huweza kuchubua sehemu hizo na kufanya urahisi wa maambukizi.
- Vaa nguo za ndani asili ya pamba na zisizobana sana kuacha hewa ya kutosha ili kupunguza maambukizi.
- Usibane mkojo kila unapojisikia kwenda haja fanya hivyo ili kuepuka wadudu kusukumwa na kusambaa katika kibovu na figo.
- Usilale au kukaa kwa kukunja miguu muda mrefu kwani utawatengenezea mazingira mazuri wadudu ya kuzaliana na kusambaa sehemu za juu za mwili,
- Kondom za kike pamoja na chemikali za kuzuia mimba hupunguza kinga na huwezo wa mwili hivyo kusababisha wadudu kuongezeka.
- Dalili zikizidi muone daktari kwa ushauri na dawa ili kumaliza tatizo
KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI
No comments:
Post a Comment