Mabadiliko mengi hutokea kipindi ambacho msichana hukua kuelekea katika utu uzima kubwa zaidi likiwa ni kipindi cha hedhi chenye mabadiliko ya homoni na matatizo mbali mbali ambayo humfanya msichana au mwanamke kukosa amani na kutokujiskia vizuri. Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ambayo hutokea mara kwa mara kwa wasichana na wanawake wengi ambapo yashaelekezwa sana katika blog hii:
- Maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhoea)
Hii husababishwa na kusinyaa na kutanuka kwa ukuta wa mimba ambao hutolewa sambamba na damu inayotoka. Hali hii huweza kuzuiwa au kupunguzwa kwa kutumia dawa za kutuliza maumivu na njia mbali mbali kama ilivyoelekezwa katika blog hii.
- Kutokwa na damu nyingi kupita kiasi ( Menorrhagia)
Hapa mwanamke hutokwa na damu nyingi na kwa kasi kuliko kawaida na hubadilisha pedi au kitambaa kila baada ya saa. Pia huweza kupitisha saiku zake kutoka 5 mpaka 7 na kuendelea, mara nyingi hii husababishwa na mabadiliko ya hormoni ambayo husababishwa na maambuki ya magonjwa mbali mbali, uvimbe, kansa na utoaji wa mimba. Matibabu yake ni kutibu jambo linalosababisha pamoja na dawa za kuzui kutokwa na damu kama ilivyoelekezwa katika blog hii.
- Siku zinazobadilika (Irregular cycles)
Hii hutokea pale mwanamke anapopata siku zake mapema au kuchelewa hivyo kutokutambua tarehe maalumu. pia huweza kuambatana na kutokwa na damu chache kuliko kawaida inayoababishwa na mabadiliko ya homoni, mawazo, vidonge vya kuzuia mimba, kupungua uzito na mazoezi kupita kiasi.
- Msongo wa mawazo na hasira (Premenstrual syndrome)
Hii husababisha kukosa raha na kuwa na hasira sana hasa wiki moja kabla ya kuingia katika siku zake na huadhiri sana mahusiano mengi endapo mwenza hatokuwa muelewa wa hali hii.
- Maumivu ya kichwa na tumbo kuvimba( Headache
and bloating )
Hii husababishwa na mabadiliko ya hormoni za estrogeni na progesteroni ambazo husababisha tumbo kujaa gas, kukosa choo na na maumivu ya kichwa.
Haya mataizo ni ya kawaida kabisa kwa wanawake wengi na hutokana na mabadiliko ya homoni katika kipindi hiki lakini mara nyingine yakiwa sugu na makali kupita kiasi huweza kuwa ni ishara ya matatizo mengine hivyo kuitaji matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment