Hii ni saratani inayoshambulia njia
ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba. Ugonjwa huu ukijulikana mapema unaweza
kutibiwa, wakati wa kufanyiwa uchunguzi wa awali. WHO inakadiria kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea zaidi katika
nchi zinazoendelea.
Hali hiyo si ya kufikirika bali ni ya kweli kwani wanawake wengi wa Kitanzania
wanathibitisha hilo kwa kutoa shuhuda mbalimbali.
Nani yumo hatarini
- Wanawake wenye maambukizi ya “human papillomavirus” HPV au genital warts
- Wanawake wasioenda kwa uchunguzi wa kila mwaka wa fupa nyongo na ubwabwa
- Wanawake walioingia kwenye tendo la ndoa kabla ya wakati
- Wanawake wenye magonjwa ya zinaa kama chlamydia, gono, kaswende na Ukimwi.
- Kuvuta sigara na kutokula vyakula bora huweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi kwa kupunguza kinga ya mwili.
Dalili za awali za saratani ya
mlango wa kizazi
- Hamna dalili zozote mpaka unaposambaa nje ya mlango wa kizazi.
- Kutokwa na damu nyingi sehemu za siri hasa kwa kipindi ambacho hauko kwenye hedhi,
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kutokwa na damu baada ya tendo
- Kutokwa na ute usio wa kawaida na harufu mbaya sehemu za siri
Dalili zinazotokea baada ya saratani
kukomaa na kusambaa sehemu nyingine za mwili zinaweza kuwa
Maumivu makali chini ya kitovu au
mgongoni
Kukojoa damu au kukojoa mara kwa
mara
Kushindwa kupumua vizuri
Kupoteza hamu ya kula au kupungua
uzito
Kukosa choo au kupata choo
iliyochanganyika na damu
kuhisi
uchovu, maumivu ya nyonga, maumivu ya mguu, mguu mmoja kuvimba, kuvunjika
mifupa na kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye sehemu ya uke wa mwanamke.
Ukiona dalili hizi fika hospitali
kwa uchunguzi na ushauri wa dakta
Matibabu
Matibabu ya ugonjwa wa saratani hiyo
hutolewa kulingana na hatua za ugonjwa na hali ya mgonjwa. na njia za kutoa
matibabu ni pamoja na upasuaji katika hatua za mwanzo (Surgery),
mionzi(Radiotherapy) na dawa za
saratani( Chemotherapy)
Pia ipo huduma endelevu kwa wagonjwa wa saratani ambayo hutolewa kwa lengo la kupunguza makali na kuboresha afya kwa watu wenye magonjwa sugu, ikiwemo saratani.
Zaidi ya yote wanawake wanashauriwa kujenga tabia ya kupima mara kwa mara ili kubaini mapema endapo wana saratani na kuanza matibabu mapema kabla maradhi hayo hayajafikia hatua mbaya.
Pia ipo huduma endelevu kwa wagonjwa wa saratani ambayo hutolewa kwa lengo la kupunguza makali na kuboresha afya kwa watu wenye magonjwa sugu, ikiwemo saratani.
Zaidi ya yote wanawake wanashauriwa kujenga tabia ya kupima mara kwa mara ili kubaini mapema endapo wana saratani na kuanza matibabu mapema kabla maradhi hayo hayajafikia hatua mbaya.
No comments:
Post a Comment