Friday, 9 May 2014

TATIZO LA KUOTA NDEVU KWA WANAWAKE

Tatizo la kuota ndevu na nywele sehemu ambazo hazistaili kama kifuani, tumboni, mgongoni na usoni   huwa kero kwa wanawake na wadada wengi kutokana na  kupunguza urembo wa mwanamke hivyo kuitaji msaada na matibabu zaidi. Nywele za aina hii hujulikana kama nywele kuruwili(Hirsutism ) na husababishwa na matatizo mbali mbali katika mwili wa mwanamke




NINI HUSABABISHA? 
Hali hii husababishwa na kuwepo kwa hormoni ya kiume ijulikanayo kama testosterone ambayo husababisha kukua kusambaa kwa nywele za kiume kwa mwanamke sambamba na chunusi usoni sauti nzito na kukomaa kwa misuli ya mwanamke inayotokana na
  • kuongezeka kwa tezi ya adrenali na saratani ya tezi hii
  • Uvimbe katika via vya uzazi wa mwanamke
  • Unene na uzito kupita kiasi
  • Kuugua mgonjwa wa kisukari kwa muda mrefu
  • Dawa za steroids ambazo hutumika katika vipodozi vingi wanavotumia wanawake
  •  Matumizi mabaya ya dawa za uzazi wa mpango na kuzuia mimba.

MATIBABU YAKE
  • Kunyoa na kung'arisha sehemu yenye nywele kwa kutumia blichi na cream zisizo na steroids
  • Mchanganyiko wa dawa za Finasteride, Sipirolactone na Flutamide  hupunguza uwezo wa testosterone kufanya kazi hivyo kupunguza na kuondoa dalili hizi
  • Kufanya mazoezi ya kupunguza uzito unene pia husaidia kuondoa tatizo hili
  • Katika hospiatali zilizoendelea njia za kitaalamu huondoa nywele kwa kutumia umeme na laser
KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI
 
 



No comments:

Post a Comment

.