Friday 23 May 2014

JINSI YA KUEPUKA MADHARA YATOKANAYO NA POMBE KUPITA KIASI

Unywaji wa pombe kupita kiasi huwa na madhara makubwa sana kwa binadamu kwa muda huo  au madhara mengine huweza kutokea baadae hasa matatizo ya Ini, Figo, moyo  kibofu, ubongo na magonjwa mengine mengi. Unaweza kuepuka madhara hayo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
  • Kunywa maji mengi kabla na baada ya kunywa pombe: Hii hukuwezesha kunywa kiasi kidogo cha pombe na kuondoa kiasi kikubwa cha pombe mwilini kupitia kibofu kwa njia ya mkojo.
  • Kunywa Taratibu sana:  kwa kutambua kuwa huwezi kata kiu kwa pombe zaidi ya kupunguza maji mwilini na kukuongezea kiu zaidi hivyo kunywa haraka itafanya pombe kukuathiri baadae.
  • Usichanganye aina nyingi za pombe; ili ni kosa kubwa linalofanywa na walevi wengi ili kuongeza ladha bila kujua kuwa kila kinywaji huingia mwilini kwa kasi yake ambapo nyingine huchewa wakati nyingine huwahi.
  • Usikae sehemu moja:Kutembea tembea sehemu tofauti na kuongea na watu itakufanya ugundue pindi utakapoanza kurewa na pombe kuzidi mwilini na kuufanya mwili huwe tayari kutoa nguvu kubwa kwa ajili ya kupambana na madhara ya pombe
  • Epuka kunywa kwa mashindano; hii inaweza kuonekana sifa au furaha mbele za watu wakati ikikuathiri kwa upande mwingine kwa kunywa pombe nyingi ambazo zitaingia haraka katika mifumo ya mwili pamoja na damu na kusababisha madhara makubwa.
  • Kumbuka chakula pamoja na matunda: hii itasaidia mwili kuwa na nguvu kupunguza madhara ya pombe pamoja na kuongeza nguvu wakati matunda husaidia kutoa vitamins ili kulinda ubongo usiharibiwe na pombe. Kumbuka wakati mwingine pombe huweza kukosesha hamu ya kula hivyo kukufanya utegemee zaidi matunda na Vitamins complex ambazo hupatikana hospitalini na maduka ya madawa
  • Tambua kiasi cha pombe kinachokufaa: hii itasaidia mwili kujijenga wenyewe kwa ajili ya kutumia kiasi hicho cha pombe bila madhara yoyote sambamba na kuepuka aina ya pombe inayokusumbua
  • Pata usingizi wa kutosha: hakikisha unakula chakula cha kutosha na kunywa maji mengi kabla ya kulala ili kupunguza uchovu na kurudisha mwili katika hali ya kawaida


KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI






No comments:

Post a Comment

.