Sunday, 25 May 2014

FAIDA NA AINA MBALIMBALI ZA MASAJI.




Masaji ni tiba mojawapo inayoweza kukusaidia kupunguza uchovu, maumivu, kupumzisha akili  na kurekebisha  mzunguko wa damu. Zifuatazo ni aina za masaji ambazo unaweza kufanya ili kuweka mwili wako katika hali nzuri

Saturday, 24 May 2014

MATATIZO AMBAYO HUWAPATA WANAWAKE WENGI KIPINDI CHA HEDHI(PERIOD)

Mabadiliko mengi hutokea kipindi ambacho msichana hukua kuelekea katika utu uzima kubwa zaidi likiwa ni kipindi cha hedhi chenye mabadiliko ya homoni na matatizo mbali mbali ambayo humfanya msichana au mwanamke kukosa amani na kutokujiskia vizuri. Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ambayo hutokea mara kwa mara kwa wasichana na wanawake wengi ambapo yashaelekezwa sana katika blog hii:
  • Maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhoea)
Hii husababishwa na kusinyaa na kutanuka kwa ukuta wa mimba ambao hutolewa sambamba na damu inayotoka. Hali hii huweza kuzuiwa au kupunguzwa kwa kutumia dawa za kutuliza maumivu  na njia mbali mbali kama ilivyoelekezwa katika blog hii.
  • Kutokwa na damu nyingi kupita kiasi ( Menorrhagia)
Hapa mwanamke hutokwa na damu nyingi na kwa kasi kuliko kawaida na hubadilisha pedi au kitambaa kila baada ya saa. Pia huweza kupitisha saiku zake kutoka 5 mpaka 7 na kuendelea, mara nyingi hii husababishwa na mabadiliko ya hormoni ambayo husababishwa na maambuki ya magonjwa mbali mbali, uvimbe, kansa na utoaji wa mimba. Matibabu yake ni kutibu jambo linalosababisha pamoja na dawa za kuzui kutokwa na damu kama ilivyoelekezwa katika blog hii.
  • Siku zinazobadilika (Irregular cycles)
Hii hutokea pale mwanamke anapopata siku zake mapema au kuchelewa hivyo kutokutambua tarehe maalumu. pia huweza kuambatana na kutokwa na damu chache kuliko kawaida  inayoababishwa na mabadiliko ya homoni, mawazo, vidonge vya kuzuia mimba, kupungua uzito na mazoezi kupita kiasi.
  • Msongo wa mawazo na hasira (Premenstrual syndrome)
Hii husababisha kukosa raha na kuwa na hasira sana hasa wiki moja kabla ya kuingia katika siku zake  na huadhiri sana mahusiano mengi endapo mwenza hatokuwa muelewa wa hali hii.
  • Maumivu ya kichwa na tumbo kuvimba( Headache and bloating )

Hii husababishwa na mabadiliko ya  hormoni  za estrogeni na progesteroni ambazo husababisha tumbo kujaa gas, kukosa choo na na maumivu ya kichwa.
 Haya mataizo ni ya kawaida kabisa kwa wanawake wengi na hutokana na mabadiliko ya homoni katika kipindi hiki lakini mara nyingine yakiwa sugu na makali kupita kiasi huweza kuwa ni ishara ya matatizo mengine hivyo kuitaji matibabu zaidi.


KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI
 











Friday, 23 May 2014

JINSI YA KUEPUKA MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO (U.T.I)

Ugonjwa katika njia ya mkojo (U.T.I) ni ugonjwa unaoshambulia njia za mkojo na husipotibiwa au kuchukuliwa tahadhari mapeme huweza pia kushambulia kibofu na figo hatimaye kuleta madhara zaidi. Ugonjwa huu hutimbiwa kwa kutumia mchanganyiko wa  dawa tofauti ambazo hutolewa kwa ushauri wa daktari.

MADHARA YA KUPIGA PUNYETO



Ili tuweze kuongezeka inatubidi tuzaliane kama viumbe wengine, na hatuwezi tu kuzaliana bila ya kujamiiana, na hatuwezi kujamiiana bila ya kuwa na hisia zitakazotupelekea kufanya kitu kama hicho. Katika maumbile ya mwanadamu hupata hisia hizo anapofikia umri wa kubalehe na ndio hapo huanza kuona mambo mageni kiasi cha kumfanya ajione tofauti na wengine hata kama nao

JINSI YA KUEPUKA MADHARA YATOKANAYO NA POMBE KUPITA KIASI

Unywaji wa pombe kupita kiasi huwa na madhara makubwa sana kwa binadamu kwa muda huo  au madhara mengine huweza kutokea baadae hasa matatizo ya Ini, Figo, moyo  kibofu, ubongo na magonjwa mengine mengi. Unaweza kuepuka madhara hayo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
  • Kunywa maji mengi kabla na baada ya kunywa pombe: Hii hukuwezesha kunywa kiasi kidogo cha pombe na kuondoa kiasi kikubwa cha pombe mwilini kupitia kibofu kwa njia ya mkojo.
  • Kunywa Taratibu sana:  kwa kutambua kuwa huwezi kata kiu kwa pombe zaidi ya kupunguza maji mwilini na kukuongezea kiu zaidi hivyo kunywa haraka itafanya pombe kukuathiri baadae.
  • Usichanganye aina nyingi za pombe; ili ni kosa kubwa linalofanywa na walevi wengi ili kuongeza ladha bila kujua kuwa kila kinywaji huingia mwilini kwa kasi yake ambapo nyingine huchewa wakati nyingine huwahi.
  • Usikae sehemu moja:Kutembea tembea sehemu tofauti na kuongea na watu itakufanya ugundue pindi utakapoanza kurewa na pombe kuzidi mwilini na kuufanya mwili huwe tayari kutoa nguvu kubwa kwa ajili ya kupambana na madhara ya pombe
  • Epuka kunywa kwa mashindano; hii inaweza kuonekana sifa au furaha mbele za watu wakati ikikuathiri kwa upande mwingine kwa kunywa pombe nyingi ambazo zitaingia haraka katika mifumo ya mwili pamoja na damu na kusababisha madhara makubwa.
  • Kumbuka chakula pamoja na matunda: hii itasaidia mwili kuwa na nguvu kupunguza madhara ya pombe pamoja na kuongeza nguvu wakati matunda husaidia kutoa vitamins ili kulinda ubongo usiharibiwe na pombe. Kumbuka wakati mwingine pombe huweza kukosesha hamu ya kula hivyo kukufanya utegemee zaidi matunda na Vitamins complex ambazo hupatikana hospitalini na maduka ya madawa
  • Tambua kiasi cha pombe kinachokufaa: hii itasaidia mwili kujijenga wenyewe kwa ajili ya kutumia kiasi hicho cha pombe bila madhara yoyote sambamba na kuepuka aina ya pombe inayokusumbua
  • Pata usingizi wa kutosha: hakikisha unakula chakula cha kutosha na kunywa maji mengi kabla ya kulala ili kupunguza uchovu na kurudisha mwili katika hali ya kawaida


KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI






Friday, 9 May 2014

TATIZO LA KUOTA NDEVU KWA WANAWAKE

Tatizo la kuota ndevu na nywele sehemu ambazo hazistaili kama kifuani, tumboni, mgongoni na usoni   huwa kero kwa wanawake na wadada wengi kutokana na  kupunguza urembo wa mwanamke hivyo kuitaji msaada na matibabu zaidi. Nywele za aina hii hujulikana kama nywele kuruwili(Hirsutism ) na husababishwa na matatizo mbali mbali katika mwili wa mwanamke

SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI (Cervical Cancer)



Hii ni saratani inayoshambulia njia ya kizazi kati ya uke na mji wa mimba. Ugonjwa huu ukijulikana mapema unaweza kutibiwa, wakati wa kufanyiwa uchunguzi wa awali.  WHO inakadiria kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea zaidi katika nchi zinazoendelea.
Hali hiyo si ya kufikirika bali ni ya kweli kwani wanawake wengi wa Kitanzania wanathibitisha hilo kwa kutoa shuhuda mbalimbali.

MAELEZO KUHUSU UGONJWA HATARI WA DENGUE NCHINI

Dengu ni ugonjwa wa mlipuko unaosababishwa na virusi vinavoenezwa na mbu aina ya Aedes aegypti wanaouma muda wowote
kuna aina mbili za ugonjwa huu ugonjwa wa papo kwa papo (Acute)  ambao huchukua muda wa wiki moja mpaka mbili na ugonjwa wa muda mrefu(chronic) baada ya wiki mbili na kuendelea.

DALILI ZA AWALI
Dalili za ugonjwa huu ufanana sana na magonjwa ya malaria na mafua hivyo ni muhimu kuwahi hospitali zenye vipimo ili kutambua ugonjwa huu uonapo dalili hizi:
  • Maumivu sehemu za jointi na misuli
  • Kuvimba kwa tezi mbalimbali za mwili
  • maumivu ya kichwa na nyuma ya macho
  • Vipele katika sehemu za ngozi pamoja na homa kali
  • kichefuchefu na kutapika

DALILI ZA BAADAE
Endapo ugonjwa huu hautotibika mapema huweza kupelekea dalili za awali kuwa kali sana na kuingia katika hatua ya Dengue hemorrhagic fever (DHF) sambamba na maumivu makali ya tumbo kupumua kwa kasi, mwili kuchoka na kutapika damu, mshtuko na kukosa fahamu hatimaye kusababisha kifo.


MATIBABU
Kutokana na ugonjwa huu kusababishwa na virusi hakuna matibabu kamili kwa ugonjwa huu zaidi ya kutibu na kuondoa dalili za ugonjwa huu mapema ili kuzuia vifo. Maumivu, uvimbe na homa huweza kupunguzwa kwa kutumia dawa zozote rahisi za kutuliza maumivu kama paracetamol. Wakati dalili za mafua huweza kutibiwa na kutulizwa kwa dawa yoyote ya kutibu mafua na kunywa maji mengi.

.