Wanawake wengi ukabiliwa na tatizo la maumivu wanapokuwa katika siku zao ambayo kitaalamu huitwa Dysmenorrhea. Hali hii uchukuliwa kama maumivu ya kawaida kwa kila mwanamke isipokuwa yanapokuwa makali yakiambatana na dalili kama kichefuchefu, kutapika, kukosa choo na nyingine nyingi ambazo usababisha mwanamke hasifanye shughuli zake za kila siku.
Maumivu yanapokuwa makali sana chini ya kitovu na kwa muda mrefu huweza kuwa yamesababishwa na matatizo ya uzazi, magonjwa ya zinaa na U.T.I hivyo unashauriwa kumuona daktari mapema