Wanawake nchini Venezuela wanatumia kemikali haramu ijulikanayo kama “Silicon” kuongeza ukubwa wa makalio yao na kujiletea madhara makubwa ya kiafya
Hii ni kutokana na mtindo ambao unaonekana na wengi nchini humo kwamba mwanamke mwenye makalio makubwa ndiye anayependeza zaidi
Wanawake wengi sasa wanahatarisha afya zao kwa kutaka kuwa 'warembo'
Mmoja kati ya wanawake, mwenye umri wa miaka 35 ambaye pia ni wakil abubujikwa na machozi, baada ya siku moja kujikuta na uvimbe sawa na ukubwa wa mpira katika sehemu ya chini ya mgongo wake.
Daktari anaonyesha picha ya moja ya athari za sindano za Silicon kwa makalio
Sababu? Kupata kile ambacho jamii inaona kama urembo.
Sindano hizo zilipigwa marufuku na serikali mwaka 2012, miaka sita baada ya Denny kudungwa (Wakili).
Denny alidungwa sindano ya kemikali hiyo ya Silicon mwaka 2006 na leo ndio ameanza kuhisi athari zake.
Hata hivyo wanawake wengi wanaendelea kujiongezea makalio (umri wa miaka 18-50).
Utafiti unaonyesha kuwa wanawake zaidi ya kumi hufariki kila mwaka kutokana na kudungwa sindano hizo.
Kuna madaktari wawili pekee wanaoweza kumfanyia upasuaji mtu kama Danny aliyeathrika kutokana na kemikali hiyo lakini kwa Danny anahitaji kusubiri kwa mwaka mmoja kabla ya kufanyiwa upasuaji huo maana kuna wanawake wengi kwenye orodha ya wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
CHANZO: AFYA CHECK
No comments:
Post a Comment