Monday 19 January 2015

KWA WANOPENDA UREMBO BANDIA SOMA KILICHOMKUTA MREMBO HUYU

Andressa Urach mshindi wa pili katika mashindano ya mrembo mwenye makalio mazuri na miguu mizuri zaidi kupitia kwenye mtandao wa internet alidungwa sindano za kemikali ili kufanya makalio yake kuwa makubwa pamoja na kuongeza ukubwa wa miguu yake. 
Lakini mnamo mwaka 2013, mwili wake ulianza kuoza ndani.
Athari za kujiweka urembo bandia zilianza kumwandama Urach hadi madaktari wakalazimika kutoa kemikali hizo kutoka mwilini mwake mwezi Novemba kwa kuchimba mashimo katika mapaja yake.
Mwili wake ilipatwa na mshtuko kwa sababu ya ugonjwa alioupata kwa kutumia vifaa chafu vya matibabu mwilini mwake lakini madaktari waliweza kuokoa maisha yake lakini hadi leo anatumia tu kiti cha magurudumu na miguu yake ina mashimo mengi ambayo madaktari waliweza kutoboa ili kutoa kemikali zenye sumu alizotumia kuongeza ukubwa wa makalio na miguu.

No comments:

Post a Comment

.