1. Jiwekee utaratibu wa kufunga kwa siku mbili au tatu, wakati huo
ukitumia maji ama juisi ya matunda au vyote kwa pamoja. Usile chakula
kingine chochote. Faida ya kufunga ni kuondoa sumu mwilini, ambazo
mara nyingi zimekuwa chanzo cha magonjwa.
2. Wakati matibabu
yanaendelea usitumie vyakula vya kuhamasisha mwili kama chai, kahawa,
pombe, sigara, vinywaji vyote vya ‘cola’, vyakula vilivyokaangiziwa
viungo vingi, nyama, mafuta yanayopatikana kwa wanyama, vyakula vya unga
uliolowekwa na sukari nyeupe.
3. Epuka vyakula vilivyosindikwa
(tinned) kwa kuwa havina virutubisho vya kutosha. Pia madawa
yanayotumika kuvifanya vikae muda mrefu bila kuharibika yanaathiri
mwili.
4. Pata muda wa kutosha kwa ajili yamapumziko na mazoezi.
5. Usinywe maji wakati unaendelea kula. Kunywa maji saa moja kabla na baada ya mlo.
6. Kunywa maji mengi iwezekenavyo. Usinywe chini ya glasi 8 kwa siku.
7.
Tumia zaidi chakula cha mboga za majani, matunda, nafaka
zisizokobolewa, aina zote za kunde, maharage na karanga, asali na
maziwa.
8. Wakati wa usiku usikae muda mrefu ukisoma ama kutazama runinga. Mwanga usio wa asili huleta athari. Lala mapema.
9. Nenda kulala angalau masaa mawili baada ya chakula cha jioni.
10. Wakati unapokuwa umekaa ama unatembea, uti wa mgongo ukae wima.
11. Lalia godoro gumu wala siyo godoro ama kitanda kinachonesanesa.
12.
Sagisha mboga na matunda kwa ajili ya kachumbari kwa maji ya moto ama
yanayotiririka. Katakata matunda na mboga katika vipande vikubwa ili
kuepuka kupoteza vitamini muhimu na madini.
13. Usile wakati umekasirika, una wasiwasi, una woga ama una majonzi
No comments:
Post a Comment