Majengo mengi yaliyo katika ghorofa kuanzia nne na kuendelea yamekuwa yakiwekwa lift za umeme ili kusaidia watu kupanda na kushuka kwa urahisi na uharaka, nimekutana na hii story ya Gavana mmoja kuzuia watu kutumia lift ili watu wapambane na tatizo la uzito mkubwa.
Obesity imekuwa moja ya tatizo linalowakabili sana watu wa nchi za Ulaya, mwaka jana Uingereza na Hungary zilitajwa kama moja ya nchi zenye tatizo hili kwa kiasi kikubwa.
Dursun Ali Sahin, Gavana wa Jimbo la Edirne, Uturuki amepiga marufuku hiyo ili watu watumie ngazi kupanda kuanzia ghorofa ya kwanza mpaka ya tatu, ila watakaoruhusiwa ni wale tu ambao wana matatizo ya kiafya.
Majengo ambayo hayajaguswa katika agizo hilo ni Hospitali na kwenye nyumba za wauguzi peke yake
“Ukitumia
ngazi badala ya lift inakuongezea siku za kuishi… Hii ni hatua ya
kupromote afya bora… Itasaidia pia kupunguza gharama za matumizi ya
umeme…” – Sahin.
Mwaka jana Gavana huyo aliwahi kupiga marufuku matumizi ya sukari kwa wingi katika chai zinazouzwa katika migahawa.
Mitandao ya kijamii haijakosa
kuzungumzia hili, watu waliopita huko wamesema eti ujanja utakaotumika
utakuwa hivi; mtu akiwa na shida ghorofa ya tatu atajirahisishia safari
yake, atapanda lift mpaka ghorofa ya nne halafu atafanya kutembea tu
kurudi ghorofa ya tatu kwa kushuka ngazi.
No comments:
Post a Comment