Kiungulia
ni hali inayojitokeza kwa mtu kuhisi maumivu ya kuwaka moto yakianzia
maeneo ya chini ya kifua yakipanda katikati ya kifua hadi kufikia katika
usawa wa kooni.
Hali
hii ya kuhisi kuwaka moto kooni au kifuani husababishwa na tindikali au
acid iliyoko tumboni ambapo tindikali hii inakuwa inapanda juu kutoka
tumboni kutokana na matatizo mbalimbali katika mfumo wa tumbo na
miongoni mwa matatizo ni mtu kuwa na tatizo la kuzalishwa tindikali
nyingi zaidi tumboni kuliko mahitaji halisi.
Mpenzi
msomaji, kutokana na tafiti zilizofanywa, imegundulika kuwa, mtu kuwa
na kiungulia cha mara kwa mara huwa hatarini kupata tatizo la kansa ya
koo kwa asilimia 78, na hii ni kwa watu ambao siyo watumiaji wa pombe na
pia kwa wasiotumia au kuvuta sigara.
Tafiti
hizo zilizofanyika nchini marekani na kuchapishwa katika jarida maalumu
la habari za kitafiti za magonjwa ya kansa, A journal of the American
Association for Cancer Research, pia zimeeleza kuwa, dawa zinazotumika
kupunguza tindikali (Antacids) zimeonekana kusaidia kupunguza hatari ya
mtu kupata kansa ya koo inayosababishwa na kiungulia cha mara kwa mara,
lakini kwa dawa zinazotumika kuua vijidudu vinavyosababisha magonjwa,
antibiotics, hazina msaada katika kupunguza hatari hii ya kansa ya koo.
Mpenzi
msomaji, katika tafiti hiyo utaona kwamba, inawezekana mtu tatizo la
kuwa na kiungulia akaliona ni kitu kidogo sana, na hata akaacha kuchukua
hatua zinazostahili ili kuondokana na hali hiyo, lakini mwisho wake ni
kuja kupata tatizo kubwa zaidi, kansa, utahitaji muda mwingi zaidi,
gharama kubwa na kupitia matibabu magumu ili kuithibiti kansa ya koo.
Sasa
ni wakati wa kubadilika, tujiepushe na vitu vinavyoweza kuleta
kiungulia. Tuwe na utaratibu maalumu wa kula chakula kwa maana ya
kutokaa na njaa kwa muda mrefu ambapo pia itasaidia kuepuka vidonda vya
tumbo, kukiandaa chakula vizuri kabla ya kukipika mfano maharagwe ambayo
huwa na tindikali asilia nyingi, ulaji wa matunda mfano mapapai au
ndizi, kunywa maji ya kutosha hata kama hauna kiu na pia kufuata ushauri
wa wataalamu wa afya kulingana na hali yako ili kuweza kuishi katika
afya nzuri zaidi.
No comments:
Post a Comment