Saturday, 6 June 2015

UPUNGUFU WA DAMU (ANEMIA) UNAVYOWEZA KUHATARISHA MAISHA YAKO.

Upungungufu wa damu husababishwa na mambo mengi kama kupoteza damu nyingi kutokana na kuumia, hedhi, wakati wa kujifungua, magonjwa mbalimbali na maambukizi ya minyoo. Pia huweza kuchangiwa na magonjwa ya kurithi, matibabu ya mionzi, ukosefu wa lishe asa yenye madini ya chuma, folic na vitamini B12. 

Tatizo ili uhathiri zaidi wanawake, wajawazito na watoto na yafuatayo ni mambo ambayo unaweza kufanya kujilinda na tatizo ili. Kula chakula na lishe yenye madini ya chuma, folic, vitamin B na C Kujikinga na kutibiwa mapema magonjwa yanayosababisha upungufu wa damu kama malaria, minyoo, na mengineyo. Kuku, samaki, matunda na mboga za majani ni vyakula muhimu sana.

No comments:

Post a Comment

.