Wednesday, 3 June 2015

SABABU NA TIBA YA CHUNUSI WAKATI WA UJAUZITO:

Wanawake wengi husumbuliwa na chunusi wakati wa ujauzito. Hii hutokana na mabadiliko ya mwili hasa kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa ujauzito inayosababishwa na kuongezeka kwa homoni ambazo husababisha mwili kutengeneza mafuta mengi na kuyaifadhi katika sehemu za uso. Habari njema ni kwamba ili ni jambo la kawaida na uisha baada ya miezi mitatu ya mwanzo hivyo huitaji zaidi matunzo ya ziada.
Matumizi ya vipodozi kwa kipindi cha ujauzito kuondoa tatizo hili huwa si salama asa vile vyenye kemikali za hydroxy acids, retinol na salicylic acids ambavyo huweza kupenye kenye ngozi hadi kwenye damu na kumuhathiri mtoto. Vipodozi vya asili, sabuni na baadhi  ya vipodozi vyenye  antibiotics huweza kusaidia kutakatisha uso na kuondoa tatizo 
BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WAELIMISHE MARAFIKI

No comments:

Post a Comment

.