Kuvuta sigara ni tabia ambayo imezoeleka na
watu wengi ingawa ina madhara mengi Uvutaji
sigara huathiri mwili kwa njia tofauti na madhara yake ni makubwa
kiafya. Inakadiriwa kuwa, hadi sasa kumegunduliwa kemikali zipatazo
7,000 katika moshi wa sigara ambapo 250 kati ya hizo ni sumu na 70
zinasababisha kansa.
Mvutaji mdogo hutumia nusu ya pakiti ya sigara kwa
siku na kujikuta akiathiri mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa
mwaka. Mada na kemikali zilizo kwenye sigara huathiri karibu kila kiungo
mwilini kuanzia seli hadi mfumo wa kulinda mwili.
Kemikali zilizoko
kwenye moshi wa sigara huingia katika mapafu na kuenea katika mwili
mzima na kusababisha madhara makubwa kwa njia mbalimbali. Ingawa mada
hizo haribifu zilizoko kwenye moshi wa sigara ni nyingi, lakini tatu ni
hatari zaidi zikilinganishwa na nyingine. Mada hizo ni nikotini, carbon
monoxide na tar.
BOFYA HAPA KUJUA MARADHI MENGINE YANAYOSABABISHWA NA SIGARA
No comments:
Post a Comment