WATU
23 wamepoteza maisha na wengine 34 wamejeruhiwa usiku wa kuamkia
leo baada ya gari aina ya costa mali ya Another G inayofanya safari
zake kati ya Njombe na Iringa kugongana na Lori mkoani Iringa.
Ajali
hiyo imetokea eneo la Kinyanambo nje kidogo na mji wa Mafinga wilaya
ya Mufindi mkoani Iringa wakati gari hiyo ya Another G ikitokea
Iringa kwenda Njombe
Mkuu
wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo
na kueleza kuwa ni miongoni mwa ajali mbaya kutokea wilayani
Mufindi .
No comments:
Post a Comment