Monday, 15 June 2015

JINSI YA KUPAMBANA NA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI (PERIOD)

Wanawake wengi ukabiliwa na tatizo la maumivu wanapokuwa katika siku zao ambayo kitaalamu huitwa Dysmenorrhea. Hali hii uchukuliwa kama maumivu ya kawaida kwa kila mwanamke isipokuwa yanapokuwa makali yakiambatana na dalili kama kichefuchefu, kutapika, kukosa choo na nyingine nyingi ambazo usababisha mwanamke hasifanye shughuli zake za kila siku.
Maumivu yanapokuwa makali sana chini ya kitovu na kwa muda mrefu huweza kuwa yamesababishwa na matatizo ya uzazi, magonjwa ya zinaa na U.T.I hivyo unashauriwa kumuona daktari mapema.
Unaweza kufanya yafuatayo ili kuepuka, kupunguza na kuondoa maumivu haya:
  • Weka kitambaa chenye joto kiasi au barafu chini ya tumbo
  • Chua na kanda kwa kuzunguka sehemu ya chini ya kitovu kwa kutumia ncha za vidole
  • Kunywa vinywaji vya moto
  • Kula chakula kidogo na mara kwa mara chenye carbohydretes, matunda nafaka na mboga za majani
  • Epuka vyakula vyenye sukari na chumvi nyingi, pombe, Kahawa na sigara
  • Lala kwa kunyanyua miguu juu au upande na huku umekunja miguu
  • Fanya mazoezi mara kwa mara
  • Kama maumivu hayapungui unaweza tumia dawa kama paracetamol, ibuprofen, diclofenac na vitamin B6 au muone daktari kupata msaada zaidi.

No comments:

Post a Comment

.