Tuesday, 16 June 2015

SOMA MADHARA YA SMARTPHONE NA UYAEPUKE

Wataalamu wa macho wanashauri kuwa matumizi kupindukia ya mara kwa mara ya simu za kisasa (Screen touch Smartphone), TV pamoja na Computer yana madhara sana kwa afya ya macho kutokana na kuwa na mionzi ya Blue violet ambayo huweza kusababisha upofu wa macho.

Pia matumizi ya muda mrefu ambayo husababisha kuharibu au kukosa usingizi husababisha athari za kisaikologia kama mawazo, hasira na wasi wasi unapokuwa mbali na simu yako.
Pia matumizi ya muda mrefu wa simu za kisasa husababisha maumivu ya kichwa, shingo, na mabega kutokana na kupunguza mzunguko wa damu katika sehemu hizi.
Hata hivo tunashauriwa kufanya uchunguzi wa macho mara kwa mara ili kugundua matatizo haya kabla hayajafikia katika hatua ya upofu ambayo huwa ngumu na ghalama kutibika.

No comments:

Post a Comment

.