Tuesday 16 June 2015

TAHADHARI KWA WANAWAKE WANAOFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE.

Ni kweli washauri wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, ili uweze kumshika vilivyo mpenzi wako unatakiwa kuhakikisha unampa katika kila anachokitaka lakini hawakuzungumzia ishu ya wewe kukubali mapenzi kinyume na maumbile. Hawakurusu hilo kwa kuwa wanajua madhara ya kufanya hivyo. Sasa iweje leo ukubali kufanya dhambi hiyo eti kwa kuwa mpenzi wako kataka na unampenda?

Katika ulimwengu wa sasa wapo wanaume wa ajabu sana. Hawa ni wale ambao si wastaarabu. Wao hawaangalii madhara yanayoweza kuwapata wenzao bali wanaangalia kujifurahisha wao tu. Mbaya zaidi baadhi ya wanawake nao wamekuwa mbumbumbu.
Eti kwa kuogopa kuachwa au kusalitiwa wanasema bora wafanye hivyo. Jamani, ifike wakati tufikirie kila tunalolifanya katika maisha yetu ya kila siku. Zipo mbinu nyingi za kumridhisha mpenzi wako na wala asifikirie kukuacha wala kukusaliti bila hata kumkubalia afanye hivyo.
Pia unatakiwa kufahamu kwamba, unaweza kumpa mpenzi/mume wako mapenzi hayo lakini bado akakusaliti tu. Sasa kwa nini ujidhalilishe?

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI. 

No comments:

Post a Comment

.