Zinaa ni
miongoni mwa magonjwa ambayo yanaongezeka kila siku na sababu kubwa ni
jamii kutokuwa na utaratibu wa kupima afya mapema na hivyo kuchelewa
kupata matibabu sahihi. Matokeo yake ni kusababisha madhara makubwa.
Warts ni miongoni mwa magonjwa hayo. Watu wengi waliopatwa na ugonjwa huo hawaonyeshi dalili zozote.
Daktari
bingwa wa Magonjwa ya Uzazi na Ngozi wa Kituo cha Magonjwa ya Maambukizi
(IDC), Dk Goodluck Mushi anasema ugonjwa wa Warts unaoambukizwa kwa
njia ya kujamiiana.
Dk Mushi
anasema Warts kwa jina jingine ni nyama zinazotokea sehemu za siri
katika uume au uke au ndani ya uke pia katika haja kubwa sehemu ya
pembeni au katika mashavu ya ukeni.
Ugonjwa wa
Sunzua ama warts husababishwa na virusi aina ya Human Papilloma (HPV),
ambavyo husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya
kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni.
Anasema mbali na sehemu hizo pia sunzua hutokea pembeni ya mdomo au katika ulimi.
Anasema kati ya watu 100 wenye magonjwa ya zinaa, 40 wana virusi vinasababisha ugonjwa huo wa warts.
Anasema asilimia kubwa ya watu wanaougua ugonjwa huo ni wanawake kutokana na maumbile yao.
Kwa upande
wa mwanaume anapata kutokana na michubuko na hivyo virusi hivyo huingia
katika njia ya mkojo na mwanaume anaweza kumwambukiza mwanamke kwa
kumwagia mbegu.
Hali ikoje mikoani?
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Watoto kutoka Hospitali ya Wilaya ya Bariadi, Dk
Nicholas Mbasa anasema kati ya wanawake 200 ambao walifika katika
hospitali hiyo kutibiwa asilimia 38 waligundulika kuwa na ugonjwa wa
Warts katika kipindi cha mwaka 2013 pekee.
Dk Mbasa
ambaye pia ni specialist wa Magonjwa ya kifua kikuu na ukoma anasema
tatizo la ugonjwa huo linaongezeka kila siku kutokana na uelewa mdogo
kwa baadhi ya jamii.
Anasema
baadhi ya wanaume walio katika ndoa ambao huomba kufanyiwa tohara katika
hospitali hiyo, wengi wao wanakutwa na ugonjwa huo na kuanzishiwa
matibabu.
Mikakati kuukabili
Dk Mbasa
anasema moja kati ya mikakati inayoendelea kwa nchi nzima ni katika
kupambana na ugonjwa huo ni kutoa elimu na kuhamasisha jamii kwenda
katika vituo vya kutolea tiba kwa ajili ya uchunguzi na tiba sahihi.
“Vilevile
tunaendesha kampeni za tohara kwa wanaume kwani wanaume wanaotahiriwa
hupunguza uwezekano wakupata warts kwa asilimia 77 hadi 95, huku upande
wa maambukizi ya VVU, mwanamume ambaye amefanyiwa tohara hupunguza
uwezekano wa kupata VVU kwa asilimia 60,” anasema.
Kundi hatarini
Daktari
bingwa wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kutoka Kliniki ya
MediCorps, Francis Makwabe anasema watu walio na umri kuanzia miaka 14
hadi 35 wapo katika hatari ya kupata ungojwa huo hususan wanawake
waliovunja ungo na wale walikatika umri wa kuzaa.
Dk Makwabe
anasema wenye mimba wapo katika hatari ya kupata sunzua kwa sababu mama
mjamzito anakuwa na upungufu wa kinga ya mwili.
Vilevile,
anasema wagonjwa wa kisukari wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huo
kutokana na kupungua kwa kinga ya mwili pamoja watu wanaotumia dawa
kali. Kundi jingine lililopo katika hatari ya kupata warts, analitaja ni
la wale wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo, kuwa na mpenzi zaidi ya
mmoja na kufanya ngono kinyume cha maumbile.
Mbali na kundi hilo vilevile watoto wadogo wanaweza kuambukizwa ugonjwa huo kwa kufanyiwa vitendo vya ubakaji.
Dalili zake:
Moja kati
ya dalili za ugonjwa huo ni kuwa na vinyama au vinyuzi nyuzi mithili ya
taulo laini katika sehemu za siri ambapo mara nyingi huwasha wakati wa
joto au unaponyoa nywele sehemu za siri.
Vinaweza kuota pia kwenye ulimi, mashavu ya uke, mapajani, katika lips za mdomo na usoni.
Vinyama hivyo pia vinaweza kutokea usoni, hasa sehemu karibu na kope ama maeneo mengine kama vile vidole vya miguu na mikono.
Madhara
Warts
inaweza kubainika kwa vipimo vya maabara. Warts zikitokea katika shingo
ya kizazi, inaelezwa kuwa inasababisha saratani ya kizazi kwa wanawake
na kwa upande wa wanaume inasababisha kansa kwenye sehemu ya njia ya
mkojo.
Anasema mtu
wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi yupo katika hatari ya kupata
ugonjwa huo kwa sababu nyama hizo huota na kukua kwa haraka kutokana na
upungufu wa kinga iliyoshuka.
CHANZO: MZIZI MKAVU
No comments:
Post a Comment