Athari
za magonjwa ya ngono ni pamoja na kuharibika mimba mara kwa mara, mimba
kutunga nje ya mfuko wa uzazi, ugumba, kuziba kwa mirija ya uzazi,
madadiliko ya hedhi, kujifungua kabla ya mimba kutimiza muda wake, kansa
ya uume,
kupungua nguvu za kiume, utasa, kuziba njia ya mkojo, magonjwa
ya akili na maambukizi katika kokwa za mbegu za uzazi.
Kwa upande wa watoto magonjwa haya
husababisha mtoto adumae, uambukizo wa macho, upofu, kuzaliwa na uzito
pungufu pamoja na vichomi.
Ili kujiepusha na magonjwa ya ngono, ni vyema mtu ukachukua
tahadhari hizi, kuepuka ngono katika umri mdogo, kutumia kondomu wakati
wa kujamiiana, kujiepusha na vitendo vya ubakaji. Pia ni vizuri kama
unatibiwa magonjwa haya, basi na mwenzi wako pia umpeleke akapatiwe
matibabu.
No comments:
Post a Comment